Sunday, December 23, 2012

MWANDISHI ANAHOJI SUALA LA MWALIMU NYERERE M KUWA MTAKATIFU

Mwandishi Rashid Mtagaluka
TANGU Makao Makuu ya Kanisa Katoliki duniani Vatican yaridhie ombi la Askofu wa jimbo la Musoma Mhashamu Justine Samba kutaka Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Burito Wanzagi Nyerere atangazwe kuwa MTAKATIFU, watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali kadhaa huku baadhi wakihoji mantiki ya kiongozi wa kisiasa kutunukiwa tuzo ya DINI!!

Mbali ya kuwepo kwa makundi ya kijamii kuhoji hayo, lakini pia wapo baadhi ya watu wamepata kueleza kwa undani sababu za Kanisa Katoliki kubariki ‘UTAKATIFU’ wa Nyerere.

Mmoja kati ya hao ni mwandishi wa habari wa gazeti la The Saturday Standard la Kenya Bwana Daud Kahura ambaye amepata kuandika juu ya kadhia hiyo katika toleo la April 8, 2006 ambalo binafsi nimefanikiwa kuinasa nakala yake.

Katika makala yake ndefu kwenye gazeti hilo Kahura anasema kwamba nanukuu; “Wakatoliki huwapa utakatifu watu ambao walikuwa mihimili ya kanisa waliofanya kazi kama wachungaji, watawa au watumishi wa kanisa katika kazi za kujitolea”.
Anaongeza kusema kuwa “Mwalimu Nyerere hakuwa mmoja kati ka hao, (sasa) kwanini kanisa katoliki likawa na shauku kubwa ya kumtangaza mtakatifu?”


Baada ya uchambuzi wake mrefu na kutoa mifano mingi, Kahura anasema hivi; Kwa Mwalimu Nyerere ilikuwa UKATOLIKI KWANZA na utaifa baadae… Kahura anaendelea kubainisha katika makala yake hayo kuwa; Mara kadhaa Mwalimu Nyerere alikuwa akifanya mikutano ya siri na viongozi wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kuwafahamisha kuwa; Katika baadhi ya nafasi katika TANU ameweka watu sio kwa ajili ya elimu na sifa zao la!, lakini kwa UKATOLIKI wao ili kulinda maslahi ya Kanisa Katoliki ndani ya chama.

Mwandishi Kahura anaendelea kuchambua na kusema kuwa, Mwalimu Nyerere hakufanya kazi hiyo kwa kubahatisha, bali alikuwa ameandaliwa kabla ya uhuru. Mwandishi anawataja baadhi ya watu walioshiriki kumwandaa Nyerere;

Maaskofu wa Marykhnoll Fathers (The Catholic Foreign Mission of America. Pia anawataja maaskofu wa kikatoliki waliofanya kazi ya kumwandaa Mwalimu Nyerere kuwa ni pamoja na Fr. William Collins, aliyemfungisha ndoa na mama Maria mwaka 1953, Fr. Nevins, Fr. John Considine, Fr. Arthur Wille, Fr. Richard Walsh, Fr. Collins, Nevins na Considine ndio waliomlipia nauli Mwalimu Nyerere ya kwenda Umoja wa Mataifa New York mwaka 1956.

Kwa kuthamini mchango wa Mwalimu Nyerere katika kuujenga Ukatoliki Tanzania, Kahura anafafanua Fr. Arthur Wille alikuwa miongoni mwa watu wachache waliokuwapo ubavuni mwa Mwalimu Nyerere alipokuwa katika kukata roho huko London mwaka 1999.


Aidha mwandishi Kahura anaendelea kutuhabarisha habari za ndani za namna alivyokuwa akionekana Mwalimu Nyerere na baadhi ya viongozi wa nchi mbalimbali kwa kumnukuu Waziri Mkuu wa zamani wa Singapore Bwana Lee Kuan Yew akisema kuwa; “Nyerere alikuwa MKATOLIKI KWELIKWELI, lakini asiyejua japo mambo mepesi kabisa ya uchumi”, kwa mujibu wa Kahura, Lee alitoa matamshi hayo mwaka 2001.

Pamoja na kazi kubwa ya kutukuka aliyoifanya ya kuujenga UKATOLIKI nchini Tanzania, makala ya The Saturday Standard yanaarifu kuwa; Mwalimu Nyerere alipeleka ukereketwa wake wa Ukatoliki nje ya mipaka ya Tanzania, ambapo Nyerere inasadikika alishiriki katika mauaji ya watu zaidi ya Milioni moja katika vita vya Biafra vilivyodumu kwa takriban miaka minne huko nchini Nigeria.

Makala hayo yanaendelea kuchambua kwamba, Askofu Laurent Magesa wa Musoma anaripoti kwamba, Nyerere aliungana na kundi la waasi la Kanali Chukwuwemeka Odumegwu Ojukwu kwasababu walikuwa wakatoliki wenzake. Wakatoliki hao wa jimbo la Biafra ambao ni wa kabila la Igbo walikuwa wanataka kujitenga kutoka serikali Kuu ya Nigeria.

Alifanya hayo huku Nyerere akiwa hakujali umoja wa kitaifa wa Nigeria kama tunavyoambiwa hapa Tanzania kwamba Nyerere aliupigania kwa kuujenga na kuutetea umoja wa Tanzania. Na hapa ndipo mpasuko ulipoanzia kwa Waislamu kuhoji kuwa; hivi Utaifa unaodaiwa kuwapo hapa nchini ni pale tu Wakristo wanapokuwa juu ya wengine wakipewa kila aina ya upendeleo, na inapodaiwa kutendeke haki sawa wao huja juu na kudai huo ni UDINI na kuvunja umoja wa KITAIFA alioujenga Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere?

Huku tukihimizwa Tuzingatie “Unity in diversity”. Tupige vita “Diverstiy in Unity”. Tusitangulize tofauti zetu, bali tutangulize umoja wetu!
Mimi sielewe jamani, naomba jaziba na mihemko ya kiimani visitamalaki katika kujadili mada hii. Tuangalie ‘UTAIFA ZAIDI!!!’ KARIBUNI.

No comments: