Wednesday, November 21, 2012

WACHIMBAJI MADINI MKOANI GEITA WASEMA WATAIBURUZA SERIKALI MAHAKAMANI

Story ya Dan Kaijage
KIKUNDI cha umoja wa wachimbaji  wadogo wadogo wa madini ya dhahabu (Shilabela Gold Mining Co-operative Society  Limited) katika eneo la Lulembela Wilayani Bukombe Mkoani Geita wametishia kuiburuza serikali mahakamani kama hawatapewa leseni ya uchimbaji madini.
Hatua hiyo inatokana na kile ambacho wanasema kuwa inawezekana Ofisi za serikali zinaendeshwa kiujanja ujanja na utapeli hususani katika Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwapendelea wachimbaji wakubwa na kuwakandaniza wachimbaji wadogo.
Akizungumza na Tanzania Daima Katibu wa umoja huo Felisian Anthony, alisema kuwa serikali kupitia Wizara ya nishati na Madini wanatakiwa kuingilia kati utoaji wa lesemi kwa wachimbaji hao kwani wametimiza vigezo vyote amavyo walitakiwa kutimiza kwa mujibu wa maelekezo ya maofisa Madini.
Alisema kunaonekana kuwepo kwa dalili mbaya ya kutaka kuwazunguka waombaji hao jambo ambali mpaka sasa linawafanya waombaji hao kukata tama na kujikuta wakiendelea kuwa masikini wa kutupwa wakati maeneo yao yana madini.
“Sisi ni wazawa na maeneo yetu yana madini na ndiyo maana tuliamua kutumia maeneo yetu kuomba kuchimba kwa kufuata taratibu zote lakini hapa kuna mchezo ambao unataka kuchezwa ili tusipate leseni ya uchimbaji na hili haliwezi kuvumilika “ alisema katibu.

Alisema kikundi hicho chenye wanachama zaidi ya 97 waliomba kuchimba madini katika maeneo ambayo ni mashamba yao kwa kuzingatia sera ya madini ya kumtaka mzawa ambaye yupo katika eneo lake akigundua kuwa kuna madini anaweza kufuata taratibu na kuweza kuchimba.
Kwa mujibu wa maelezo ya Anthony alisema kutoka na sera hiyo wanachama hao kwa kushirikiana walibaini maeneo yao ambayo wanaishi yalikuwa na madini ya dhahabu hivyo kuamua kufanya taratibu za kuomba leseni kama wachimbaji wadogo ili waanze kuchimba madini hayo wakiwa na matumaini ya kujikwamua kiuchumi.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo walianza mchakato wa kufuatilia eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuomba usajili wa eneo hilo mwaka juzi (2011) na kufanikiwa kupata cheti cha usajili.
Alisema kuwa mnamo Ocktoba tisa 2011 walikwenda katika ofisi ya madini ya Kahama kwa ajili ya kupata utaratibu wa umilikaji wa eneo la uchimbaji wa madini na upatikanaji wa leseni.
Akitoa maelezo Katibu wa kikundi hicho alisema kuwa kutokana na juhudi zote na taratibu zilizofanywa na kikunbdi hicho Ofisa Madini Kutoka Kahama,aliyemtaja kwa jina la Nkya, alikubaliana na wanachimbaji hao na kuwataka walipie ada ya upimaji ambayo ilikuwa ni shilingi laki mbili abayo ililipwa kwa viwanja 10 ambavyo ni sawa na heka 50.
Kikundi kiliendelea na kufanya taratiu zote ambapo kiliweza kulipa ada hiyo  ya upimaji na kupewa cheti cha usajili wa kumiliki eneo la uchimbaji No SHR 1500 ambayo ilitolewa Septemba 2011 ambayo na ikiwa na maelezo ya kuwataka watume barua ya kuomba leseni kwa ajili ya kuanza uchimbaji kutokana na Ofisa Madini kujiridhisha na kudai kuwa eneo hilo linafahaa.
Hata vyo Anthony alisema kuwa walishangazwa na barua iliyoandikwa yenye Kumb: Na.DA.230/264/03 ambayo ilikuwa ikidai kikundi hicho hakiwezi kupewa leseni kwa kuwa eneo waliloomba linapishana na maombi ya leseni ya utafiti mkubwa ya Machi 11 2009 yenye Kumbu.Na. HQ-P20025.
“Hapa hatuelewi na kamwe hatuwezi kuelewa sisi tulioma maeneo hayo kwanza ni maeneo yetu ambayo tunayamiliki kwa shughuli za uzalishaji wa kawaida, lakini pia tulianza kufanya maombi mwaka 2011 na taratibu zote zikafuatwa, tukapewa hata cheti cha kumiliki pamoja na kulipia ada ya upimaji kwa mujibu wa maelezo ya ofisa madini kutoka Kahama….
“Leo hii tunapokea barua kuwa tayari kuna maombi ya utafiti mkubwa katika eneo hilo ambayo yaliombwa mwaka 2009 kwa maana hiyo ofisi ya madini na wizara yake wakanafanyaje kazi bila kuwa na uhakika ama ofisi za serikali kwa sasa zinatumika katika kutapeli “ alihoji Anthony ambaye ni katikabu wa kikundi hicho.
Mbali na hilo alisema kinachowatia shaka ni kuona kuwa wao wameomba eneo hilo la uchimbaji na kwa kufuata taratibu zote hata risti za malipo wanazo lakini kwa mijibu wa barua iliyoandikwa na Humphrey Mmbando ambaye ni Kamishina Msaidizi wa Madini kanda ya kati Magharibi haina hata muhuri wa Wizara wala hata ofisi hiyo ya jambo ambalo linaonekana kutengenezwa.
Kwa upande wake Mbunge wa Bukombe Profesa Kulikoyela Kahigi (Chadema)alisema kuwa kwa sasa kuna kila sababu ya sheria ya Madini kuboreshwa zaidi ili iweze kuonyesha wachimbaji wadogo ambao madini yanapatikana katika maeneo yao wanapewaje leseni.

“Tatizo ni kuwa wachimbaji wadogo wanakosa kupewa vipaimbele zaidi na hapo awali haikuwepo sera ambayo inaonekana kuwatambua zaidi wachimbaji wadogo na ili kuondokana na migogoro ya wachimbaji wakubwa na wadogo nilazia waonekane wanafanya nini katika kuhakikisha wanachimba bila kukumbana na kero mbalimbali” alisema.

Pamekuwepo na malalamiko mengi kwa wachimbaji wadogo kunyanyashwa, hata hivyo kwa suala hili ambalo linaonekana kuleta sura ya mgogoro inawezekana ikawa ni matatizo ambayo yanweza kukuzwa pasipo kuwa na sababu kama waombaji waliomba katika kipindi cha mwaka 2011 na kutimiza vigezo vyote na kupewa cheti cha kumiliki lakini kumbe alikuwepo mwombaji mwingine tangu 2009 kulikuwa na haja gani kuwapa matumaini waombaji hao wadogo.

No comments: