Story ya www.dankaijage.blogspot.com
MBUNGE wa mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu
amesema kuwa kwa sasa nguvu zake za kutuliza vurugu za watu wanaotaka kuteka
magari ya mafuta jijini hapo.
Mbilinyi amesema kuwa kutokana na tatizo
la mafuta nchini wakazi wa jiji la Mbeya kwa sasa wameanza fujo za kutaka
kuteka magari ya kusafirisha mafuta kwenda nchi za jirani.
Kwa mujibu wa Mbilinyi alisema kuwa hali
hiyo inatokana na msimamo wa serikali kudai kuwa hakuna tatizo la mafuta nchini
wakati katika jiji la Mbeya tatizo hilo ni kubwa na kupelekea nauli ya daladala
kupanda ktoka shilingi 500 hadi kufikia shilingi 1500.
“Mimi kama mbunge jiji Mbeya ambaye
nimekuwa nikijitahidi sana kutuliza ghasia za wananchi wangu pindi inapotokea
machafuko kwa hili sasa nimeshindwa” alisema Sugu.
Mbali na hilo alisema hali hiyo
inasababishwa na serikali kutokuwa na uwazi katika masuala mazima ya kutoa
taarifa za ukweli kwa wananchi na pale inapotokea matatizo kama hayo.
Hivi karibuni ulitokea sokomoko kubwa
ambalo lilipelekea kuzuka kizaa zaa bungeni.
Kutokana na kizaa zaa hicho cha mafuta
kilipelekea, WAZIRI kivuli wa
Nishati na Madini, John Mnyika , kuibana serikali akitaka itoe kauli kuhusu
uhaba wa nishati ya mafuta uliyoikumba nchi, baada ya kushindwa kufanya hivyo
licha ya kuwa iliahidi.
Pia ilipelekea
hoja hiyo ilitikisa bunge baada
ya Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Kangi Lugola, alipoibua hoja ya kutaka Bunge
lisitishe shughuli zake na badala yake wabunge wajadili tatizo hilo.
Pamoja na hoja
hiyo ya Lugola na Maelezo mazuri ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene kwamba tatizo hilo limekwisha, Spika
wa Bunge, Anne Makinda alimuagiza Waziri wa Nishati na Madini kulitolea tamko
rasmi suala hilo jana.
Hata hivyo
katika hali ya kushangaza, serikali ilishindwa kutoa tamko huku Waziri wa
Nishati na Madini pamoja na Naibu wake wote wakiwa hawapo Bungeni.
Kutokana na
kushindwa huko kwa serikali, hali hiyo ilimlazimu Mnyika ambaye pia ni Mbunge
wa Ubungo kuomba muongozo akitumia
Kanuni ya Bunge ya 68 (7) kuhoji kwa nini serikali imeshindwa kuliweka
suala hilo kwenye ratiba ili Mawaziri watoe tamko kuhusu tatizo la mafuta.
Pamoja na hilo,
Mnyika alimshutumu Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Simbachawene kwa
kulieleza Bunge uongo kwamba tatizo la
mafuta limekwisha wakati bado lipo.
“Napigiwa simu
na watu wananiambia kwamba tatizo la mafuta bado lipo, Waziri alieleza uongo
kwamba tatizo la mafuta hakuna naomba serikali ieleze kuhusu hilo” alisema
Mnyika.
Mbali na hilo
Mnyika pia aliwashangaa Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo
kutofautiana kauli na Naibu wake, Simbachawene kuhusu
kumalizika kwa tatizo hilo huku mwingine akisema bado.
Baada ya kauli
hiyo ya Mnyika, ilimlazimu Spika Makinda kumpa nafasi Waziri Mkuu alitolee
ufafanuzi kutokana na kutokuwepo kwa Waziri
wa Nishati na Madini wala Naibu wake.
Kuhusu hilo,
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliahidi serikali kutoa tamko kabla ya shughuli za
Bunge hili hazijakwisha.
Pamoja na hilo
Pinda pia alikiri Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Waziri wake kutoa kauli
za kutofautiana huku
akilihakikishia Bunge kuwa serikali itatoa kauli yake.
Hata hivyo Pinda
alisema kuwa tatizo la mafuta mikoani lisigeweza kumalizika kwa siku moja au
mbili kwa sababu matanki yakijazwa na yakianza kupelekwa huchukua muda kidogo.
Ijumaa iliyopita
wakati Mbunge Lugola akitoa hoja yake ya kutaka Bunge lijadili tatizo la mafuta
alisema hali ya upatikanaji wa mafuta jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa
imekuwa mbaya, kiasi cha kuwafanya watu kupata nishati hiyo kwa vibaba.
Lugola alisema
ana wasiwasi na tatizo
linachochewa na hujuma inayofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wa mafuta ambao
wanataka kukwamisha mpango wa Serikali wa kuagiza mafuta kwa pamoja (Bulk
Procurement).
“Hujuma
zinafanyika kuonyesha mfumo wa ununuzi wa namna hii si mzuri ili Serikali irudi kwenye mfumo wa zamani wa kuagiza mafuta ya reja reja ili wao wafaidike
zaidi.
“Ninaomba Bunge
lako tukufu liahirishe shughuli zake ili tuweze kujadili jambo hili na ninaomba
wabunge wote waniunge mkono”.
Hoja hiyo
ilipoungwa mkono, Spika wa Bunge, Anne Makinda alimtaka Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo kutoa kauli ya Serikali juu ya tatizo hilo.
Hata hivyo kauli
ya Serikali ilitolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
ambaye alisema tatizo hilo limekwishashughulikiwa.
Wakati akitoa
kauli hiyo jana, Profesa Muhongo hakuwapo bungeni kwa maelezo kuwa yupo Dar es
Salaam akijadiliana na wadau wa mafuta katika kutatua tatizo hilo.
Akielezea chanzo
cha tatizo hilo, Simbachawene alisema ni uzembe uliofanywa na baadhi ya
watendaji katika Idara, Mamlaka na Taasisi za Serikali zilizopewa jukumu la
mafuta.
Aliwataja
wanaohusika na uzembe huo ni Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA),
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mratibu wa ununuzi wa mafuta kwa jumla
(PIC).
Simbachawene
alisema watendaji hao waliruhusu meli zenye mzigo wa mafuta kwa ajili ya nchi
jirani kutia nanga bandarini, bila kujua kiwango cha akiba ya mafuta kilichopo
hapa nchini.
“Tatizo hili
tumelishughulikia tumechukua mafuta yaliyokuwa yakipelekwa nchi jirani na
kuyafungulia hivi sasa Dar es salaam imekwishajaa mafuta na sasa yanatoka huko
na kwenda mikoani” Alisema na Spika kumtaka atoe kauli ramsi ya serikali jana.
No comments:
Post a Comment