Thursday, November 8, 2012

MBURAHATI QUEENS YACHANGIWA NA WABUNGE


Story ya www.dankaijage.blogspot.com

WABUNGE wanawake wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), jana wamekabidhi kiasi cha shilingi laki tano kwa mbunge wa Ubungo John Mnyika kwa ajili ya kuchangia Timu ya Mburahati Queens.

Akikabidhi mchango huo Waziri kivuli wa Wizara inayoshughulikia michezo Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu alisema kuwa hali hiyo imetokana na hali ya kitu hiyo kueleza jinsi inavyokutana na magumu pindi walipotembelea  bunge kwa ajili ya kuona shughuli za bunge zinavyoendelea.

Sugu alisema kuwa kimsingi kuna kila sababu ya kuhakikisha timu za wanawake zinapigwa tafu kwani timu nyingi zinazofadhiliwa ni timu kubwa wakati timu kama za mburahati Queens zinaachwa pembeni.

Alisema kuwa kutokana na wabunge wanawake kuonyesha hali ya kuwatia moyo wachezaji wa timu hiyo ni njia mojawapo ya wabunge, wafadhili pamoja na wadau mbalimbali wa michezo kuchangia kwa kiasi kikubwa michezo ya jinsi hiyo.
Kwa upande wake mbunge wa Ubungo John Mnyika ambako timu hiyo inatokea alisema kuwa amefurahishwa na kitendo cha wabunge wanawake kutoa michango yao kwa hali na mali kuwezesha kuichangia timu hiyo.
Pia ameiomba serikali kuhakikisha inaweka sera zake vizuri kwa ajili ya kusaidia timu mbalimbali kama hiyo kwani timu hiyo imekuwa timu maarifu na imekuwa ikizalisha wachezaji wengi hata katika timu ya Twiga stars wanatokea katika timu hiyo.
Mbali na hilo alisema kuwa kuna kila sababu ya serikali kutumia fedha ambazo zinatoka FIFA kuwafikia wachezaji wa timu zote ikiwemo timu ya Mburahati Queens ambayo kwa sasa inafanya vizuri na wanafanya michezo kwa kwa kujituma na kujenga heshima ya michezo nchini.

No comments: