Sunday, November 18, 2012

STORY ZILIZOMALIZIA WIKI HILI KI CCM ZAIDI HIZI HAPA

Zimeandikwa na Danson Kaijage,(www.dankaijage.blogspot.com)

MUNGE wa Bukombe, Profesa Kulikoyela Kahigi ameieza mikakati ya chama cha Mapinduzi (CCM)kwa kudai kuwa kwa sasa hakiwezi kurudisha heshima yake kutokana na kupoteza mwelekeo wa kw watanzania.
Profesa kahigi kizungumza na tanzania Daima akiwa safrini kuelekea jimoni kwake alisem pmoj na mjigambo ya viongozi wa chama hicho kujinadi kuwa wana mpango wa kurudish heshima ya chama hicho ni kujisumbua kwani hakuna jipya ambalo wanaweza kuwaeleza watanzania wakawaelewa.
Alisema kuwa kinachodhihilisha kuwa chama hicho hakina uwezo wa kurudisha heshima kwa watanzania ni kutona na kutoheshimu katia ya chama hicho ambayo ilikuwa na misingi ya ujamaa pamoja na azimio la Zanzibar.
Mbli na hilo Profesa Kahigi alisema kuwa jambo jingine ambalo linaonesha wazi kuwa serikali ya chama cha mapinduzi  haiwezi kurudisha heshima ni kutokana na kushindwa kutekeleza mipango yake na kutumia muda wao mwingi kuwadanganya watanzania.

Alisema kwa sasa serikali imekuwa ikijinadi kwa madai kuwa elimu ni bure kwa shule za msingi na sekondari wazazi ama walezi kuchangia kidogo jambo ambalo si la kweli na matokeo yake wazazi wenye watoto wamekuwa wakichangishwa fedha nyingi zaidi ya maelekezo ya serikali ya CCM.


Alisema kauli za serikali kudai kuwa wanafunzi wa kitanzania amao wapo shule za msingi wanapatiwa elimu bure ni uongo kwani wazazi na walezi wa wanafunzi hao wanalazimika kuchangia michango mbalimbali mingi na kusababisha wazazi ama walezi kukata tamaa na kujikuta wakiacha shule.
“Katika suala la elimu kwa sasa kuna tabaka kubwa, angalia watoto wa wakubwa hawasomi katika shule za kata wao wanasoma shule nzuri za watu binafsi ama wanasoma shule za nje ya nchi na wale ambao wanasoma shule za kata ki watoto wa watanzania amao hawana uwezo….
“’Kutokana na hali hiyo kamwe serikali ya CCM haiwezi kurejesha heshima kwa watanzania kwani hakuna jipya ambalo linafanyika tofauti na kutengeneza matabaka kati ya watanzania wenye uwezo na wale ambao hawana uwezo” alisema
Akizungumzia upande wa afya alidai kuwa kwa sasa suala la afya ni gumu kwani, viongozi wa serikali walio wengi wanapata matibabu nje ya nchi ama katika vituo, Zahanati na Hospitali za viwangi vya juu wakati watanzania wenye kipao cha chini wamekuwa wakienda kutibiwa katika vituo hivyo ambavyo havina hata dawa.
Akizungumzia matambo ya CCM kudai kuwa wamepata sekretariet nzuri ya CCM ni kujidanganya kwani wapo viongozi wengi ambao wana madaraka lakini walishiriki kuwaingiza wabunge wala rushwa bungeni.
“Hakuna mtu ambaye anaweza kujidanganya huyo sekretariet iliyoteuliwa naijua vizuri hakuna mtu msafi licha ya kuwa umri wao ni mkubwa lakini hata katika mambo yao ambayo yanahusika na tuhuma mbalimali za ubadhilifu.
Hata hivyo hivi karibuni Mwenyekiti wa CCM taifa Rais Kikwete alitama kuwa kutokana na timu ambayo imechaguliwa ni timu ya ushindi ambayo itafanya kazi kubwa ya kushambulia nchi nzima kwa ajili ya kujenga chama hicho na kurejesha heshima ya chama kwa wanachama na wasio wanachama.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

JK AWASUTA WABAYA WA CCM

IKIWA ni siku chache baada kufanyika kwa uteuzi wa Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwenyekiti wa Chama hicho  Taifa, Jakaya Kikwete amewashambulia  wanachama wa chama hicho ambao walikuwa na ndoto za kufikiri kuwa mkutano mkuu uliofanyika Kizota mjini hapa ungemalizika katika sura ya mpasuko na machafuko.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akitoa hotuba yake ya kuwatamburisha rasm viongozi wa Sekretariet ya chama hicho ambayo iliwateua baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa CCM juzi.
Alisema kuwa anawashangaa baadhi ya wanachama ambao wanakifahamu vizuri chama lakini walikuwa wakiombea mabaya ili mkutano umalizike vibaya ili waweze kujivunia kile walichokikusudia katika kuvona unatokea mpasuko.
“Namshukur u sana mungu tumemaliza salama kuna watu walikuwa wakitambiaka usiku na mchana CCM imalize vibaya mkutano wake na walitamani itoke na vipande lakini wameshindwa na sijui watamdai nani gharama zao …..
“Lakini nataka niwaamibie kuwa wamepoteza muda wao bure na CCM Imara imeweza kumaliza mkutano wake vizuri na kupanga safu ya ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kuingia Ikulu mwaka 2015” alisema Rais Kikwete.
Alisema kuwa pamoja na mambo mengine yote waliokuwa wakiombea Mkutano wa Chama hicho ni wale ambao hawakijui vizuri chama tofauti na ilivyo kwa wale ambao  chama wanakijua vizuri.
Alisema kuwa wapo wajumbe ambao walikuwa wakitegemea kuwaona watu wao katika safu na sasa hawapo na waliopo ni wengine ambao watakuwa msitari wa mbele katika kukujenga chama kwa nguvu nyingi na kukifanya chama hicho kusonga mbele.
“Nimesikia mambo mengi na kuna watu kabissa walikuwa wakinijia wakiniambia kuwa kuna jambo hili na hilo, lakini nilikuwa nawaambia kuwa tulia kuna watu wana ndoto za mchana wanatumia nguvu nyingi , wanatumia muda wao bure na wanapoteza wakati  wao” alisema
Mbali na hilo Rais Kikwete alitamba kutekeleza maazimio ambayo wameyaazimia moja baada ya linguine ili kuhakikisha wanayatimiza kwa wakati na kwa muda mfupi ili watanzania waweze kuendelea kujenga imani na chama hicho.
Alisema kila mapendekezo ambayo yalitolewa na kila kanda katika kuwasiliza mapendekezo katika mkutano mkuu yatapitiwa kwa umakini na yatafanyiwa kazi na kuhakikisha yanatimizwa kwa wakati na kwa muda mwafaka.
“Na mapendekezo hayo yatafanyiwa kazi mapema ili utekelezaji wake uweze kuitekelezeka katika kipindi cha NEC ya kwanza ambayo itakutana katika kujadili mambo mbalimbali ambayo mkutano Mkuu umeazimia kufanya..
“Na hiyo itafanywa na kamati Kuu ya NEC ambayo itakuwa na mchanganyiko wa watu mahiri ambao ni wasomi na watu wenye ujuzi mbalimbali kulingana na uteuzi utakavyokuwa umefanyika ili kuhakikisha kila kitengo kimekamatwa na watu ambao ni waelewa na wenye ueledi wa juu katika kazi wanazo zifanya” alisema Rais Kikwete.
Alisema wajumbe wa NEC wanatakiwa kutumia muda wao mwingi kuifanya kazi ya chama ili kuweza kukijenga chama hicho kwa kiwango kikubwa.
“Wale ambao watajiona hawana kasi ya kufanya kazi ya chama kwa kutumia muda wao mwingi na wanafikiria kufanya biashara ni bora waachie na waendelee na biashara zao kwa sasa tunaitaji kujenga chama kwa nguvu na kuzunguka nchi nzima ili kuhakikisha tunapata ushindi wa kishindo kuanzia serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu na baadaye tunapumzika Ikulu kupanga safu ya uongozi wa serikali inayoongozwa na CCM…
“Wajumbe wa NEC ambao wanapenda kufanya biashara waendelee na biashara zao tutaweka watu wengine, wajumbe wa NEC wachemke nchi nzima kujenga chama , na ili kuweza kufanya vizuri kwa sasa yatatolewa mafunzo kwa viongozi wote kuanzia ngazi ya shina hadi taifa “ alisema Kikwete.

1 comment:

MIGONGO1950 said...

CHANGIA MAONI YAKO MDAU, KATIBA INAKURUHUSU KUTOA MAONI, ILA KUMBUKA WAJIBU WA HAKI YAKO...KARIBU SANA