Friday, November 16, 2012

KWA WALE WENYE MAPENZI MEMA , MTOTO HUYU ANAHITAJI MSAADA



MILIONI 
sita zinahitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto Selemani Said (1), 
ambaye anajisaidia haja kubwa kupitia utumbo mkubwa huku ukiwa nje ya 
tumbo lake imeleezwa.

Akizungumza
na wandishi wa habari Katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo),jijini
Dar es Salaam leo, mama wa mtoto huyo, Veronika Laurent ambaye ni Mkazi
wa Bunju, alisema mtoto huyo alizaliwa huku akiwa na sehemu ya kutolea 
haja kubwa lakini cha kushangaza, haja kubwa ilikuwa ikitokea mdomoni.

Alisema 
msaada wa fedha hizo utasaidia katika kumfanyia operesheni mtoto huyo 
ambaye kwa sasa anaishi akiwa katika mateso makubwa.
Veronika alisema hivi sasa yeye pamoja na mwanaye huyo wanaishi maisha ya
kubahatisha baada ya baba wa mtotohuyo kuitelekeza familia hiyo kutokana
na hali ya ugonjwa wa mtoto huyo.
Aidha,
alisema hadi utumbo wa mtoto huyo kutoka nje, ni baada ya kufanyiwa
operesheni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo hata
alipompeleka tena kwa ajili ya matibabu alikosa ushirikiano kutoka kwa
madaktari na wahudumu wengine.


Alisema

kwa yeyote ambaye yuko tayari kumsaidia anaweza wasiliana naye kwa
kupiga simu namba o715 83 77 00, na namba ya mwenyekiti huyo wa mtaa
0656780236.

No comments: