Tuesday, November 20, 2012

ALIETUHUMIWA KWA WIZI WA MIFUGO AUAWA, MUSOMA

Story ya Ahmad Nandonde

Ahmad, Mwandishi wa story
MTU mmoja anadhaniwa kuwa ni mwizi wa mifugo,ameuawa kwa kukatwa katwa kwa mapanga pamoja na kuchomwa mikuki na wanayowe wa kijiji cha Gentamome wilayani Serengeti mkoani Mara baada ya kuiba ng’ombe 200 za wananchi wa kijiji hicho.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw Elisha Sinda,amesema kuwa mtu huyo akiwa na wenzake zaidi ya watano waliiba ng’ombe hizo zikiwa malishoni wakati zikichungwa na watoto wawili wa kijiji hicho jana jioni.

Amesema baada ya kuiba ng’ombe hizo waliwateka watoto hao kwaajili ya kusaidia kuziswaga lakini baadae mtoto mmoja alifanikiwa kutoroka kisha kutoa taarifa kwa wananchi ambao walipiga simu kijijini hapo kwaajili ya kutoa taarifa za tukio hilo.

Bw Sinda amesema baada ya yowe kufuatilia nyayo za mifugo hiyo,waliwakuta wezi hao wakiwa na ng’ombe hizo karibu na daraja la Murito wakielekea wilaya ya Tarime na hivyo kuanza mashambuzi makali kwa kutumia silaha za jadi ambayo yalizaa matunda kwa kumuua mtu huyo huku wangine wakitoroka jambo ambalo limewawezesha kuokoa mifugo hiyo na mtoto ambaye alitekwa.

Kwa sababu hiyo mwenyekiti huyo wa kijiji cha Gentemome,ameiomba serikali kujenga vituo vya polisi katika vijiji vya pembezoni vinavyopakana na nchi jirani ya Kenya kwani amesema mara nyingi wezi hao wamekuwa wakitoka nchi hiyo jirani kisha kushirikiana na baadhi ya raia kwaajili ya kufanya uhalifu huo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo wa kijiji,mwili wa mtu huyo tayari umechukuliwa na polisi wa kituo kikuu cha mjini Mugumu wilayani Serengeti ambao walifika muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea.

No comments: