MBUNGE wa Bukombe, Profesa, Kulikoyela Kahigi ameitaka serikali kuhakikisha inatenga maeneo ya malisho ya mifugo ili kuondokana na migogoro inayojitokeza kati ya wakulima na wafugaji.
Kauli hiyo aliitoa baada ya wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kunaweza kutokea machafuko kati ya wakulima a wafugaji.
Hali hiyo inatokana na wafugaji kukosa maeneo ya kuchungia mifugo yao na wakati mwingine kujikuta wanachungungia mifugo yao katika mashamba ya wakulima.
Hata hivyo wafugaji hao wanadai kuwa wanakosa sehemu ya kuchungia na pale awanapopeleka mifugo yao kuchunga wanakamatwa na maofisa mali asili na kuwatoza faini kubwa na pale wanaposhindwa kutoa faini mifugo yao uchukuliwa ama kupigwa risasi.
Mmoja wa wafugaji ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini kwa ajili ya usalama wake na mifugo yake aliwatuhumu maofisa wa mali asili kuwa wamekuwa wakiwaomba rushwa wafugaji hadi milioni 5 pale mifugo yao inapokutwa ikichungia katika maeneo ambayo yametengwa kama hifadhi .
“Hapa hatuna sehemu ya kulishia mifugo na tunalazimika kupeleka mifugo yetu katika maeneo ambayo yanasemekana kuwa ni hifadhi, mbali na hilo tunajikuta tukigombana na wakulima pale ambapo mifigo yetu inaingia katika mashamba yao na hii yote ni shauri ya serikali” alisema mfugaji huyo.
Aidha alisema kuwa ili kumalizika kwa matatizo hayo anamwomba Waziri wa Maliasili Balozi Khamisi Kagasheki kutembelea wafugaji katika Wilaya ya bukombe ili aweze kujionea hali halisi ya jinsi wafugaji wanavyotozwa rushwa na maofisa mali asili na mpaka sasa mifugo hiyo iko maporini.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo Profesa Kulikoyela Kahigi (Chadema)alithibitisha kuwepo kwa tatizo hilo kati ya wafugaji, wakulima na maofisa wa mali asili.
Alisema licha ya kuwa suala hilo tayari alisha lipeleka bungeni kwa waziri mwenye dhamana lakini bado mambo mengi yanachukuliwa kisiasa badala ya kufanya utatuzi wa kutosha ili wananchi waweze kuishi kwa amani na kuboresha mifugo yao na kilimo kwa ujumla.
Hata hivyo aliwataka wafugaji kupunguza mifugo yao kwa kuiuza ili wapate fedha na waweze kuanzisha miradi mbalimbali kwa ajili ya kukuza kipato chao.
Kwa upande wa Maofisa wa mali asili walipotafutwa ili waweze kujibu tuhuma za kuwatoza rushwa wafugaji hao na kuthibitisha kama kweli mpaka sasa katika maeneo ya hifadhi kuna mifugi hawakuweza kuatikana huku baadhi ya watu ambao walidai kuwa siyo wasemaji wakidai kuwa wapo katika opareisheni.
No comments:
Post a Comment