Sunday, November 25, 2012

FAMILIA YAAPA KULIPIZA KISASI KWA JESHI LA POLISI , USHIROMBO

HALI imezidi kuwa tete katika jeshi la polisi kituo cha Ushirombo kutokana na familia kuapa kulipiza kisasi kwa jeshi la polisi mjini hapo kutokana na mauaji ya kinyama ambayo yaliyofanywa na askari polisi kwa kumfyatulia risasi na kumuua hapo hapo kijana ambaye alifahamika kwa jina la Rashidi Juma (23).
Mauaji hayo ambayo yalifanyika juzi katika maeneo ya Kilima hewa kwa askari wa jeshi la polisi katika kituo cha Ushirombo Mkoani Geita ambaye amefahamika kwa jina la PC Emma G4 tofauti na ilivyokuwa imesemekana kuwa muuaji ni Manase familia kwa sasa imedai kuwa jeshi la polisi linatakiwa kuwajibishwa.
Mauaji hayo ambayo yalitokana na sakata la jeshi la polisi kumshika Mabura Mayala (40)ambaye anatuhumiwa kwa ujambazi kutokana na kujificha kati ya nyumba ambazo zipo maeneo hayo.
Kwa mujibu wa maelezo ya askari polisi pamoja na wananchi zinaeleza kuwa baada ya wananchi kubaini kuwa kuna mtu ambaye walimjengea mashaka walipiga simu polisi kwa lengo la kuomba masaada wa polisi ili akamatwe.

Hata hivyo habari zinasema kuwa baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo wananchi walianza kupiga kelele na kulitaka jeshi la polisi lililohusika na kumkamata mtuhumiwa huyo kumwacha ili wananchi waweze kujichukulia hatua ya kumpiga na kumuua jambo ambalo lisingekuwa rahisi kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa shuhuda ambao waliona tukio hilo ndopo askari tajwa alipoamua kumlenga risasi kijana huyo ambaye alimpiga risasi katika sehemu ya nyonga na kumuua hapo hapo.
Kwa upande wa kamanda  wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita, (RPC) Lenard Paul, alipoulizwa kama kuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa dhdi ya mtuumiwa wa maujaji ya raia alisema kuwa askari huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi.
RPC pia alisema kuwa pindi uchunguzi utakapo kuwa umekamilika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa kuwa hakuna mtu yoyote ambaye yupo juu ya sheria lakini pia hakuna mtu ambaye anaruhusiwa kutoa uhai wa mtu mwingine.
Kwa upande wa mbunge wa Bukombe, Profesa Kulikoyela Kanalwanda Kahigi aliwataka wananchi pamoja na ndugu wa marehemu kuwa na subira juu ya tukio hilo na kuwaahidi kulishughulikia tatizo hilo hadi mwisho wake.
“Ndugu zangu wana Bukombe tunajua kuwa jeshi la polisi linafanya madudu mengi mimi ni msomi nataka niwaambie hakuna mtu anayeweza kujidanganya kwa hili, nitahakikisha nalishughulikia na mimi nimejitoa helahi kwenu kuhakikisha tatizo hili linapatiwa ufumbuzi …..
Nataka niwaabie huyo askari aliyehusika nilazima achukuliwe hatua na katika jambo kubwa kama hili hakuna siasa ambayo inaweza kujiingiza hatuingizi siasa katika jambo kubwa kama hili na wala hakuna uongo uongo ambao unaweza kujitokeza naomba mtuamini mimi na diwani wenu, Soud Ntanyagalla (Chadema)tutafanya kazi” alisema Profesa Kahigi.
Wakati huo huo kuna taarifa ambazo zinasema kuwa katika eneo la Katome wananchi ambao wanavunja sheria kwa kujichukulia sheria mikononi wamemuua mtu mmoja kwa madai kuwa ni wizi.
Inasemekana kuwa wananchi wa eneo la katome katika mji mdogo wa Ushirombo wananchi hao walimvamia mtu mmoja na kumuua kwa madai kuwa ni mwizi jambo ambali hata hivyo kamanda wa polisi Mkoa wa Geita hakuwaeza kilithibitisha kwa madai kuwa hana taarifa na hatalifanyia kazi.

No comments: