Sunday, November 25, 2012

MARA WAJIANDAA KUJENGA HOSPITALI YA RUFAA

Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA

UONGOZI WA MKOA WA MARA UMEANZA KUFANYA MAZUNGUMZO NA SHIRIKA LA HIFADHI YA JAMII NSSF KWAAJILI YA KUENDELEZA UJENZI WA MAJENGO YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MARA YALIOKO KATIKA ENEO LA KWANGWA NJE KIDOGO YA MANISPAA YA MUSOMA.

HOSPTALI HIYO AMBAYO ITAJULIKANA SASA KAMA MWALIMU NYERERE MEDICAL CENTRE,UJENZI WAKE ULISIMAMA MIAKA YA THEMANINI IKIWA NA GHOROFA MOJA BAADA YA KUKOSEKANA KWA FEDHA ZA UJENZI,AMBAPO HADI KUKAMILIKA INATARAJIWA KUWA NA CHUO KIKUU CHA MADAKTARI,WAUGUZI NA WATALAAM WENGINE WA KADA YA AFYA PAMOJA NA KITENGO MAALUM CHA KUTIBU MAGONJWA YA FIGO NA KUBADILI PALE INABIDI KUFANYA HIVYO.

MKUU WA MKOA WA MARA BW JOHN TUPPA,AMEWAMBIA WAJUMBE WA KAMATI YA AFYA YA MSINGI PHC MKOANI MARA,KUWA AWALI KATIKA KUENDELEZA MAJENGO HAYO MKOA ULIPANGA KUTAFUTA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 13,LAKINI BAADA YA KUFANYA TATHIMINI YA KINA SASA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 37 KINAHITAJIKA KWA AWAMU YA KWANZA YA UJENZI HUO.

AMESEMA UJENZI HUO UNAFANYIKA IKIWA NI SEHEMU YA UTEKELEZAJI WA AHADI YA RAIS JAKAYA KIKWETE AMBAYO ALIITOA WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010 KWAAJILI YA KUHAKIKISHA HOSPITALI HIYO SASA INAJENGWA NA KUKAMILIKA IKIWA NI SEHEMU YA KUMUENZI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS NYERERE NA KWAMBA TAYARI SERIKALI IMEANZA KUTENGA FEDHA ZA KAZI HIYO HUKU MKOA UKIFANYA JITIADA ZA KUTAFUTA WAFADHILI MBALIMBALI WA KUUNGA MKONO JUHUDI HIZO WAKATI MAZUNGUMZO NA NSSF YAKIENDELEA.

AIDHA MKUU HUYO WA MKOA WA MARA,AMESEMA KUWA TAYARI UONGOZI WA MKOA WA MARA UMECHUKUA HATUA YA KUANDAA HARAMBEE KUBWA YA KUCHANGISHA FEDHA KWAAJILI YA UJENZI WA HOSPITALI HIYO YA RUFAA AMBAYO ITAFANYIKA MIEZI MICHACHE IJAYO.



No comments: