Sunday, November 25, 2012

WATOTO 90 ELFU KUPEWA CHANJO MPYA MARA


Story ya Ahmad Nandonde , MUSOMA

ZAIDI YA WATOTO ELFU 90 WENYE UMRI CHINI YA MWAKA MMOJA MKOANI MARA WANATARAJIA KUPEWA CHANJO MPYA YA ROTAVIRUS NA NIMONIA KWAAJILI YA KUWAKINGA NA MAGONJWA YA KUHARA,UTI WA MGONGO,MAGONJWA YA MASIKIO NA VICHOMI.

MRATIBU WA CHANJO MKOANI MARA BW BEATUS RUKONA,AMEWAAMBIA WAJUMBE WA KIKAO CHA KAMATI YA AFYA MSINGI NGAZI YA MKOA KUWA CHANJO HIYO YA KWANZA KUTOLEWA NCHINI AMBAYO IMEGHARIMU KIASI KIKUBWA CHA FEDHA ITAANZA KUTOLEWA KUANZI JANUARI MOSI MWAKANI HUKU AKISEMA MAANDALIZI YA ZOEZI HILO MUHIMU YANAENDELEA VYEMA KWA KUTOA MAFUNZO KWA WOTE WATAKAHUSIKA NA KAZI HIYO.

KWA UPANDE WAKE MRATIBU WA CHANJO NA VIFAA KATIKA MPANGO WA TAIFA WA CHANJO WA WIZARA YA AFYA NA USTATAWI WA JAMII BW WILLIAM MSIRIKALE,AMESEMA KITAIFA ZOEZI HILO LINAZINDULIWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE JIJINI DAR ES SALAAM DESEMBA NNE MWAKA HUU KWA KUSHUHUDIWA NA WAHISANI MBALIMBALI AMBAO WAMETOA FEDHA KWAAJILI YA KUFANIKISHA KUTOLEWA KWA CHANJO HIYO NCHINI.

AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO HICHO MWENYEKITI WA KAMATI HIYO YA AFYA YA MSINGI AMBAYE PIA NI MKUU WA MKOA WA MARA BW JOHN TUPPA,AMEAGIZA WATENDAJI NA VIONGOZI WA NGAZI ZOTE WA MKOA HUO KUCHUKUA HATUA AMBAZO ZITAWEZESHA ZOEZI HILO KUFANIKIWA HUKU AKIOMBA VIONGOZI WA SIASA NA MADHEHEBU YA DINI KUSAIDIA KUHAMASISHA WAZAZI KWA KAZI HIYO.

No comments: