Friday, November 9, 2012

PINDA ASEMA KATIBA MPYA NI KABLA YA UCHAGUZI 2015

Story ya Dan Kaijage , Dodoma.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda jana ameliahakikishia bunge kuwa ifikapo uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 tayari katiba mpya itakuwa imekamilika.
Pinda alitoa kauli hiyo kutokana na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe (Chadema),kuitaka serikali kutoa kauli bungeni ni lini itafanya marekebisho ya katiba kuhusu kurekebisha daftari la kudumu la mpiga kura.
Mbowe alisema kuwa kutokana na daftari lakudumu la mpiga kura kupitwa na wakati kunapelekea watanzania wengi kukosa haki yao ya kupiga kura katika chaguzi mbalimbali ambazo zinaendelea tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliopita.
Hata hivyo alimtaka Wazri Mkuu kutoa kauli ya serikali kama kuna mpango wowote wa kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazoongoza uchaguzi iwapo katiba mpya ambayo inakusudiwa kutumika mwaka 2015 itakuwa bado haijakamilika.
Mbowe alisema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa katiba mpya ambayo inatakiwa kuandikwa na kutumika katika mwaka 2015 na iwapo marekebisho hayo hayatafanyiwa marekebisho ni ya sheria ya uchaguzi kuna watu wengi watakosa haki zao za kupiga kura kama ilinavyojionyesha katika chaguzi ndogo.
Aidha kiongozi huyo alitaka Wazri Mkuu atoe kauli bungeni ni lini marekebisho ya Daftari la kudumu la mpiga kura litarekebishwa ili kuweka mfumo mzuri ambao unawapa fursa wapiga kura wote wenye shifa kushiriki.

“Nakumbuka Waziri Mkuu mnamo 19 Aprili mwaka huu nilikuuliza juu ya kauli ya serikali ni jinsi gani itarekebisha daftari la kudumu la mpiga kura ili kutoa fursa kwa wapiga kura wenye sifa kushiriki lakini hadi sasa hakuna sijui kama kuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa” alisema.
Mbowe alisema kama, katiba itakuwa haijakamilika na kulazimika kufanya uchaguzi kwa kutumia katiba ya sasa kuna watu ambao watanyimwa haki zao isipokuwa tu kama kutakuwa kumefanyika marekebisho ya sheria zinazosimamia uchaguzi.
Waziri Mkuu akijibu swali hilo alisema kuwa hakuna sababu ya mbunge huyo kuwa na wasiwasi kwani ana uhakika kuwa ifikapo kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2015 katiba mpya itakuwa tayari na itatumika.
“Mimi sina shaka juu ya tatiba mpya kuwa tayari mwaka 2015 kwani hata hivi tu nilikuwa na mwenyekiti wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya Jaji Jaji Joseph Warioba na kunihakikisha kuwa kazi inaenda vizuri…..
“Hivyo mheshimiwa Mbowe sijui kwanini unakuwa na hofu lakini hata hivyo tunashukuru kwa ushauri wako kama ikionekana kujitokea kuwepo kwa mapungufu mbalimbali hadi katiba mpya isiwe tayari basi tutarekebisha sheria zinazosimamia uchaguzi ili kila mmoja apate haki yake ya kupiga kura” alisema.

No comments: