KIJANA aliejitambulisha kwa jina la EZEKIEL JOHN, ambae hata
hivyo umri wake umezua utata, baada ya yeye mwenyewe kueleza kuwa amezaliwa
mwaka 1982, lakini alipoulizwa tena akasema ana miaka 27, hii leo mchana
amesurika kupokea kipondo kikali baada ya kubainika jamaa huyo ni tapeli.
Kijana huyu inadaiwa kuwa amekuwa akitembea na kibali cha
makamu mkuu wa chuo utawala na Fedha wa chuo cha SAUT Mwanza,Fr Mwanjonde,
kuomba fedha kwa ajili ya kukomboa cheti chake cha kuhitimu masomo ya ufundi
ama injinia.
Kubainika kwake kumekuja baada ya jamaa huyo kukutwa na
vibali viwili tofauti huku vikiwa na viwango vya fedha tofauti pia, kibali
kimoja kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Nyamagana kilichonesha kuwa kinahitaji Tshs
350,000/- huku kile cha SAUT kikionesha kuwa anahitaji Tshs 550,000/-.
Pamoja na hayo muombaji wa msaada huyo alikuwa
anajichanganya maelezo ya wapi hasa amesoma na kuhitimu masoma yake, DVCAF Fr
Mwanjonde, anasema kijana huyo hajawahi kusoma SAUT na wala hadaiwi chochote
hapo, Mwenyewe mtuhimiwa alipoulizwa anadai kuhitimu katika vyuo hivi , SAUT,
UDOM na Chuo kimoja cha ufundi mkoani Mara. Na hapa ndipo utata ulipozuka.
Kwa sasa mtuhumiwa huyo yupo Kituo kidogo cha polisi cha
Igogo jijini Mwanza, akiwa amefunguliwa kesi namba MWS/RB/5471/2012, akituhumiwa
kwa KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA UDANGANYIFU.
|
Hapa Bw Ezekieli (aliekaa chini) akikabidhiwa nyaraka zake za kughushi alizotumia kujipatia fedha isivyoa halali |
|
Hapa Bw Ezekiel akitoa maelezo ya kujichanganya, mbeleya wanafunzi wa SAUT, hapa alikuwa nje ya ofisi ya DVCAF |
|
Askari wa chuo wakiwa wamemdhibiti |
|
Fr Maziku (aliesimama) akimhoji machache mtuhumiwa, |
|
Hapa wanahabari na wadau wakiendelea kupata maelezo kadhaa kutoka kwa Ezekiel, aliesimama (mwenye shati jekundu) ni Mbunge wa wasomi wa Filosofi, mahali ambako sakata la kubaini utapeli huo lilianzia |
|
Ndani ya Landcruiser, safari ya kuelekea Kituo cha Polisi Igogo ikaanza
Hapa Ezekieli akiwasili katika kituo cha polisi Igogo
NYARAKA ZENYE UTATA HIZI HAPA |
|
NYARAKA HIZI ZINAONESHA UTATA WA JINA LAKE , moja inaonesha JOHN EZEKIELI, na nyingine ikionesha EZEKIELI JOHN |
|
HIKI NI KIBALI CHA MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA, HATA HIVYO KIMEISHA MUDA WAKE |
|
HII NI BAJETI YAKE BWANA EZEKIELI, ALIYOTARAJIA KUITIMIZA BAADA YA KUJIPATIA FEDHA HIZO |
No comments:
Post a Comment