Saturday, November 10, 2012

MALIMBE MWANZA : MWANAMKE ATUHUMIWA KWA USHIRIKINA , ANASA ASHINDWA KUONDOKA KWENYE NYUMBA YA MT

Mwanamke alikamatwa baada ya kudaiwa kuishiwa nguvu zake za kishirikina , baada ya kwenda kwenye nyumba ambayo imezindikwa
Kwa ukaribu zaidi, 
Sehemu ya umati wa wakazi wa mtaa wa Malimbe, wakiwa wamekusanyika kushuhudia tukio
Baba mwenye nyumba, Bw Amri Yasini,
Mwandishi wa habari, akihojiana na Mwenyekiti wa Mtaa wa Malimbe, Bi Zenaida Musiba

STORY KIDOGO HII HAPA

Mwanamke mmoja anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40, hii leo asubuhi amekutwa akiwa mtupu eneo la Malimbe Nyegezi jijini Mwanza, baada ya kile kinachodaiwa kuwa ameenda kwenye nyumba ya Bw Yasini Amri kwa ajili ya shughuli za kishirikina
Mwenyekiti wa mtaa wa Malimbe Bi Zenaida Musiba, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kwamba kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo wakati alipokamatwa amesema kuwa alikuwa ametumwa kuchukua motto katika nyumba hiyo
Mmiliki wa nyumba hiyo Bw Yasini Amri , mwanamke huyo alidai kuwa ametumwa kuchukua damu katika nyumba hiyo na kwamba alikuwa ametokea mochwari ambayo hata hivyo mwanamke huyo hakuitaja
Kwa mujibu wa wenyeji wa mtaa huo hili ni tukio la kwanza kutokea kwa kipindi cha hivi karibuni, katika mtaa huo

No comments: