Saturday, November 10, 2012

JK AMZIKA ASKOFU BALINA HII LEO

LEO ilikuwa ni siku ya mazishi ya aliekuwa Askofu wa jimbo katoliki la Shinyanga Muasham Baba Askofu Alosius Balima, aliefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais wa Jamuhuri ya Muunugano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewaongoza mamia ya watu waliohudhuria mazishi ya kiongozi huyo wa kiimani ambaye uadlifu wake haukupingika na yeyote yule.
Misa na mazishi ya hayati Baba Askofu Balina yamefanyika katika Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga hii leo.
RAHA YA MILELE UMPE EBWANA, MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI....... AMINA. ..... BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mhashamu Baba Askofu Aloysious Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga wakati wa mazishi wa Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga leo.
Hapa Rais akiweka udongo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga wakati wa mazishi ya Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, Shinyanga leo. 
CHANZO PICHA: Michuzi blog na Fred Maro wa Ikulu

No comments: