Wednesday, November 21, 2012

MLINZI WA PUB AUAWA , MUSOMA

Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA

MLINZI MMOJA WA KAMPUNI YA ULINZI YA SALAMA SECURITY JOHN NYAGANYA(22) AMEUAWA KIKATILI KWA KUCHINJWA SHINGO AKIWA LINDONI KATIKA ENEO LA MKINYERERO,BARABARA YA MAJITA KATA YA KAMUNYONGE  MANISPAA YA MUSOMA MKOA WA MARA.

AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KAIMU KAMNADA WA POLISI MKOANI MARA SSP JAPHET LUSINGU AMESEMA KUWA NOVEMBA 21 MWAKA HUU MAJIRA YA ASUBUHI KATIKA ENEO LA MKINYERERO BARABARA YA MAJITA KAYA YA KAMNYONGE ULIGUNDULIWA MWILI WA JOHN NYAGANYA UKIWA UMEKATWA SHINGO

KAMANDA AMESEMA KUWA UCHUNGUZI WA AWALI UMEBAINI KUWA WAUAJI WALIVUNJA PUB YA TULIVU MALI YA PAUL KAREGE NA KUFANIKIWA KUIBA SANDUKU MBILI ZA BIA PAMOJA NA VITI SABA VYA PLASTIKI VYENYE JUMLA YA THAMANI YA SHILINGI LAKI MOJA NA ELFU SABINI NA SITA NA TAYARI JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MTU MMOA KUHUSIANA NA TUKIO HILO

KUFUATIA HALI HIYO KAIMU KAMANDA LUSINGU AMEWATAKA WANANCHI KUWA WEPESI WA KUTOA TAARIFA NA KUANZISHA VUKUNDI VYA ULINZI SHIRIKISHI KATIKA MAENEO YAO KWANI WAHALIFU WANATOKEA KATIKA MAENEO YAO

WAKATI HUO HUO MKAZI MMOJA WA BUHARE KATIKA MANISPAA YA MUSOMA ANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA PENDO MALIMA AMEJIKUTA KATIKA WAKATI MGUMU BAADA YA KUPOKEA KIPIGO KUTOKA KWA MWANAUME ANAYESADIKIWA KUWA MUMEWE

AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BI. PENDO AMESEMA NOVEMBA 17 MWAKA HUU USIKU ALIPOKEA KIPIGO HICHO BAADA YA KUPOKEA SIMU YA MTU ASIYEFAHAMIKA NDIPO MUMEWE ALIPOTAKA KUJUA NI NANI NDIPO ALIJIBU MAJIBU YASIYORIDHISHA HALI ILIYOPELEKEA MMEWE KUMPIGA HADI KUSABABISHA UBONGO KUHAMA NA SASA AMELAZWA KATIKA HOSPITAL YA MKOA WA MARA WODI NAMBA 4

No comments: