Story ya Ahmad Nandonde , MUSOMA
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoani Mara kamishina msaidizi mwandamizi Absalom Mwakyoma
kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia kwa Wanawake Mkoani Mara zinazofanyika katika kijiji cha
kitaswaka kata ya Bwiregi Wilayani Butiama zilizoandaliwa na asasi isiyo ya
kiserikali ya ABC Foundation chini ya ufadhiri wa Shirika la WiLDAF lenye makao
makuu yake Jijijini Dar es salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake,Mkurugenzi wa
ABC Foundation ambalo ni shirika la kutetea haki za Wanawake na Watoto Eustus
Nyarugenda amesema kuwa maandalizi yote kuhusiana na uzinduzi huo ambao lengo
lake ni kuzuia na kukomesha matukio ya ukatili katika jamii yanakwenda vizuri
na taari Wananchi wa kata ya Bwiregi wapo tayari kwa ajili ya kushirikiana na
shirika hilo katika siku hizo 16.
Amesema kuwa kutokana na kuendelea kujitokeza kwa matukio ya
ukatili huku mkoa wa Mara ukiwa unashika nafasi ya kwanza katika matukio ya
ukatili anaamini siku hizo 16 itakuwa ni chachu ya kutokomeza hali hiyo na
kupelekea jamii kubadilika na kuaachana na matukioa yote ya ukatili hususani
kwa Wanawake.
Nyarugenda amedai kuwa kesho novemba 26 ni uzinduzi wa siku ya
Kimataifa ya tunaweza kampeni ya zuia ukatili dhidi ya Wanawake ambapo shughuli
kama hizo zitafanyika katika maeneo mbalimbali yan Mkoa wa Mara huku kimkoa
ikifanyika Wilayani Butiama katika kata ya Bwiregi.
Amesema katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Mkoani
Mara wamealika mashirika mbalimbali yanayojishughulisha na ukatili wa kijinsia
kutoka kanda ya ziwa kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza pamoja na Bukoba huku
akiwaomba wadau mbalimbali wa masuala ya kupinga mambo ya ukatili watoe ushirikiano
katika kukomesha masuala ya ukatili.
Kauli mbiu ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mkoani Mara
inasema Funguka,Kemea Ukatili Dhidi ya Wanawake na sote tuwajibike.
No comments:
Post a Comment