Wednesday, November 21, 2012

MAJALIWA : WAANDISHI ANDIKENI HABARI ZENYE MASLAHI KWA JAMII

Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi (TAMISEMI) Kassim Majaliwa  amewataka Waandishi wa Habari wote Nchini kuandika Habari zenye maslahi kwa Jamii.
Kauli hiyo imetolewa leo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) na kujionea shughuli mbalimbali zamaendeleo zinazofanyika chuoni hapo.

Bw. Majaliwa wamehimiza wakufunzi kusoma kwa bidii kwa kuwa Soko la ajira limejaa ushindani mkubwa kwa amini juhudi na maarifa yao ndizo zitawafanya kufanikiwa kwenye maisha yao.

Pia wamewataka vijana ambao wamemaliza ngazi mbalimbali za Elimu hapa Nchini kujiunga na Taasisi za Habari ili kujifunza kuandika Habari kwa kufuata maadili ya kitaaluma hiyo kwa kuelimisha Jamii.

Aidha amewataka Halmashauri mbalimbali hapa Nchini kuanzisha mifumo ya upashaji wa Habari ili Jamii inayozunguka eneo hilo kupata taarifa mbalimbali na kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima.

Kwa upande mwingine ameupongeza uongozi wa Chuo hicho na Wanafunzi kwa ujumla na juhudi alizoona Chuoni hapa na kusema jambo hilo ni lakuigwa kwenye Halmashauri nyingine hapa Nchini.

Kwa upande wake afisa utawala wa Chuo hicho Bio Elifuraha Sambotoamesema Chuo kina utajiri mkubwa wa mawazo na shughuli mbalimbali ila kuna upungufu wa fedha kuendeleza mawazo na mbinu hizo.

Sambamba na hayo Bw. Samboto ametoa shukrani zake za dhati kwa Mh. Majaliwa kwa ahadi alizotoa juu ya kuboresha Studio Chuoni hapo na kurusha matangazo yao kwa Jamii.

Waziri Majaliwa amefanya ziara hiyo akiambatana na Mh. Ngonyani alimaarufu kama Maji Marefu Mbunge wa Korogwe Vijijini pamoja na Ahmed Juma Ngwali wa Jimbo la ziwani Zanzibar.

No comments: