Tuesday, November 20, 2012

KAMPENI YA KUMUOKOA MAMA MJAMZITO IMEZINDULIWA LEO JIJINI MWANZA


KAMPENI YA WAZAZI NIPENDENI YENYE LENGO LA KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI BARANI AFRIKA, KWA KUWAWEZESHA WANAWAKE WAJAWAZITO NA WENZA  WAO KUCHUKUA HATUA KWA AFYA YA MAMA MJAMZITO NA NA UZAZI SALAMA INATARAJIWA KUZINDULIWA LEO KATIKA VIWANJA VYA NYAMAGANA JIJINI MWANZA....

KAMPENI HIYO INAZINDULIWA HII LEO  WAKATI AMBAPO HAPA NCHINI VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI  IMEENDELEA KUONGEZEKA AMBAPO NI WANAWAKE 454 KATI YA WANAWAKE LAKI MOJA WANAOJIFUNGUA HUFARIKI DUNIA, HUKU WATOTO 51 KATI YA ELFU MOJA WANAOZALIWA HUFARIKI DUNIA....

MRATIBU WA KITAIFA WA MASUALA YA UZAZI SALAMA KUTOKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, DR KOHELETH WINANI , PAMOJA NA KUELEZEA KAULI MBIU YA KAMPENI HII , AMESEMA KUWA KAMPENI HII NI MWENDELEZO WA JUHUDI ZA KUPAMBANA NA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI HAPA NCHINI....
Mkuu wa mkoa wa Mwanza , ambae alimwakilisha waziri wa afya, kama mgeni rasmi washughuli hii, hapa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi


FUTUHI ON STAGE
Mkurugenzi wa masuala ya afya kutoka USAID, Bi Alisa Cameron
Aka Mtoto wa mkulima akiimba sahiri lake hapoooo
Regina kikuli, naibu katibu mkuu wizara ya afya
Eng Ndikilo, akisoma hotuba 
Hapa Eng Ndikilo akikabidhi zawadi kwa mama wajawazito waliohudhuria uzinduzi huo

Picha ya pamoja ya wadau wa kampeni hii
Hapa akina mama na waume zao wakifanya zoezi la kupokea ujumbe mfupi bure
KAMPENI YA WAZAZI NIPENDENI INARATIBIWA KWA PAMOJA KATI YA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, KITENGO CHA AFYA YA UZAZI NA WATOTO, MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI MALARIA, MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI NA KITENGO CHA ELIMU YA AFYA YA UMMA.....

No comments: