Tuesday, November 27, 2012

KUSHIRIKI KILIMO WILAYANI BUTIAMA, NI AMRI

Story ya Ahmad Nandonde , MUSOMA
MKUU WA WILAYA YA BUTIAMA MHE ANGELINA MABULA AMETOA AMRI KWA WANANCHI WILAYANI HUMO KUHAKIKISHA WANAJIHUSISHA NA KILIMO ILI KUWEZA KUJIPATIA HUAKIKA WA CHAKULA.
RAI HIYO IMETOLEWA KATIKA KIJIJI CHA KITASIKWA WILAYANI BUTIHAMA MKOANI MARA KATIKA UZINDUZI WA SIKU KUMI NA SITA ZA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE, AMBAPO MKUU WA WILAYA AMESEMA KUWA JAMII INAPASWA KUTAMBUA UMUHIMU WA CHAKULA HUSUSAN KWA WANAFUNZI WAWAPO MASHULENI NA KUMTAKA KILA kaya WILAYANI HUMO KUWA NA SHAMBA LISILOPUNGUA HEKARI 3 ILI KUWEZA KUWA NA UHAKIKA WA CHAKULA.
KWA UPANDE MWINGINE DIWANI WA KATA YA BWIREGI BI. NYAGETH AMEWAPONGEZA WANANCHI WA KATA HIYO KWA KUWEZA KUUKATAA MFUMO DUME NA KUMTAMBUA MWANAMKE KAMA KIONGOZI MAKINI KATIKA JAMII,NA HAKUNA UMUHMU WA KUWANYANYASA WATOTO WA KIKE KWA KUWAOZA KATIKA UMRI MDOGO.
HATA HIVYO AMEELEZEA BAADHI YA MIKAKATI WALIYOITEKELEZA KUWA NI PAMOJA NA UJENZI WA ZAHANATI KATIKA KIJIJI CHA NYASURURA,KIAGATA NA KAMGENDI NAKUONGEZA KUWA HIVI SASA YUPO KATIKA MIKAKATI MINGINE YA KUTEKELEZA MIRADI MINGINE MBALIMBALI KATIKA VIJIJI VILIVYOPO KATIKA KATA YAKE.
KAULI MBIU YA MAADHIMISHO HAYO NI FUNGUKA KEMEA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE SOTE TUWAJIBIKE.

No comments: