Story za Idrisa Bandali, MTWARA
Serikali imesema imeyapokea malalamiko ya wananchi wa Mtwara ya kupinga kusafirishwa gesi asili inayochimbwa mkoani humo kwenda Dar es Salaam kwa njia ya bomba.
Makamu wa Rais Dk. Mohamedi Ghalib Bilal ameyasema hayo katika ukumbi wa Veta mjini Mtwara alipokuwa anazindua mradi wa kukuza ajira kupitia vyuo vya ufundi stadi unaotekelezwa na chuo hicho kwa ushirikiano wa Britishi Gas (BG) Tanzania, na VSO ya Uingireza.
Dk Bilali amesema kuwa lazima kuwepo na mfumo wa kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafaidika gesi hiyo
Aidha amebainisha kuwa kuwa mradi huo wa miaka mitatu kuanzia mwaka huu, unalenga kuwanufaisha wanafunzi 280 ambao watakuwa wamehitimu kwa ngazi ya kimataifa na kuwawezesha kupata ajira Duniani kote.
Awali Mkurugenzi wa Mafunzo wa Veta Nchini, Bw Leah Lukindo amesema mradi huo unalenga kuwajengea uwezo wahitimu kupata ajira katika makampuni ya uchimbaji na utafiti wa gesi na mafuta ndani na nje ya nchi na hivyo kupunguza tatizo la ajira.
Kwa upande wake Meneja waBritish Gas ( BG) Tanzania, Matt Wilks amesema mafunzo hayo ya miaka mitatu yatagharimu dola za kimarekani 1milioni.
WAZEE WASTAFU
Chama chawazee wastaafu wa mkoa wa mtwara Kimeiomba jamii kubadili mitazamo finyu walioyanayo kwa wazee
Rai hiyo imetolewa hii na Katibu wa chama hicho Bw Wilbert Nandonde katika mahojianao maalumu na kituo hiki mapema hii leo
Bw Nandonde amesema kuwa wazee katika mkoa wa mtwara wamekuwa hawapati mahitaji yaliyomuhimu na ikitokea wakapatiwa huwa ni kwa kudhalilishwa
Bw Nandonde ametolea mfano huduma za afya ambazo serikali imeagiza kutibiwa bure kwa wazee Nchini kitu ambacho ameeleza ni tofauti na hali halisi iliyopo katika hospiotali zilizo nyingi Mkoani Mtwara ambazo zimekuwa zikitoa matibabu kwa wazee hao
Aidha katika hatua nyingine Bw Wilbnert ametumia fursa hiyo kuwaomba wazee ambaio hawajajiunga na Chama hicho kuhakikisha kuwa wanajiunga ili kuweza kusaidiana lkwa mambo mbalimbali
No comments:
Post a Comment