MAADHIMISHO YA SIKU 16 YA KUKEMEA NA KUPINGA UKATILI DHIDI WANAWAKE YAMEZINDULIWA HII LEO KATIKA KATA YA BWIREGI KIJIJI CHA KITASIKWA WILAYANI BUTIAMA MKOANI MARA.
AKIHUTUBIA WANANCHI WA KATA YA BWIREGI KATIKA KIJIJI CHA KITASIKWA WILAYANI BUTIAMA MKOANI MARA, KAMANDA WA POLISI KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI ABSALOM MWAKYOMA AMEITAKA JAMII KUTOFUMBIA MACHO VITENDO VYA KIKATILI DHIDI YA WANA WAKE VINAVYOFANYIKA KATIKA JAMII, IVYO AMEWATAKA WANANCHI WASIISHIE SIKU 16 BALI ZOEZI HILO LIWE ENDELEVU LISILOKUWA NA MWISHO ILI KUWEZA KUTOKOMEZA VITENDO VYA KIKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO MKOANI HAPA.
AIDHA KAMANDA MWAKYOMA AMEWAHAKIKISHIA WANANCHI UWEPO WA USHIRIKIANO WA KUTOSHA KATIKA KUPINGA ,NA KUTOKOMEZA VITENDO HIVYO,KUPITIA DAWATI LA JINSIA AMBAPO WAMEFANIKIWA KUWATIA MBALONI BAADHI YA WATUHUMIWA WANAOHUSIKA NA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE.
KWA UPANDE WAKE MWANAMKE MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FELISTER JOHN AMETOA USHUHUDA KUFUATIA KITENDO CHA KIKATILI ALICHOFANYIWA NA MUME WAKE KWA KUPIGA HADI KUPOTEZA UJAUZITO PAMOJA NA KUUNGUZWA NA PASI SEHEMU YA MGUU HALI ILIYOPELEKEA KULAZWA KATIKA HOSPITAL YA MKOA.UZINDUZI HUO ULIOHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA KITAIFA AKIWEMO MKUU WA WILAYA YA BUTIHAMA BI. ANGELINA MABULA DIWANI WA KATA YA BWIREGI,MWENYEKITI WA KIJIJI CHA KITASIKWA HUKU UKIAMBATANA NA MAONESHO YA VIKUNDI MBALI MBALI VYA WANAHARAKATI WA KIJAMII ,AMBAPO WANANCHI WENGI WALIJITOKEZA KATIKA UZINDUZI HUO.
KAULI MBIU YA MAADHIMISHO HAYO NI “FUNGUKA KEMEA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE SOTE TUWAJIBIKE”.
No comments:
Post a Comment