Story ya Ahmad Nandonde,
Wazee Mkoani Mara
Wametakiwa Kuwa Na Subira Na Kuwa Na Imani Na Serikali Wakati Matatizo Yao
Yikifanyiwa Kazi.
Hayo Yamesemwa Na
Afisa Mtendaji Wa Serikali Za Mitaa Mkoani Mara Bw, Joseph Makinga Kwa Niaba Ya
Mkuu Wa Mkoa Bw, John Tupa Katika Maadhimisho Ya Siku Ya Wazee Duniani Ambayo
Kimkoa Yamefanyika Jana Wilayani Bunda Mkoani Mara.
Bw.Makinga Amesema Ni
Wazi Kuwa Yapo Matatizo Mengi Yanayowakabili Wazee Ingawa Hayawezi Kufanyiwa
Ufumbuzi Wa Haraka Kwani Mengine Yanatakiwa Kutungiwa Sheria,Sera Ikiwa Ni
Pamoja Na Kutengewa Muda Wa Kutosha Kwaajili Ya Mapitio Ili Yafanyiwe Ufumbuzi
Pale Inapobidi.
Aidha Amewataka
Wakurugenzi Wa Serikali Za Mitaa Kuyafanyia Ufumbuzi Matizo Yaliyochini Ya
Uwezo Wa Serikali Za Mitaa Kwani Hazihitaji Fedha Za Kigeni.
Hata Hivyo Bw.Makinga
Amewataka Wananchi Kuwa Na Tabia Ya Kujiwekea Akiba Ya Chakula Ili
Kuepukana Na Kutegemea Chakula Kutoka Katika Mikoa Ya Jirani Huku Akiwataka
Kujitokeza Mchakato Wa Maoni Wa Katiba Mpya Pindi Tume Inayoundwa Na Jaji
Warioba Itakapofika Mkoani Hapa.
Awali Akisoma Risala
Kwa Mgeni Rasmi Kwa Niaba Ya Wazee Mkoani Hapa Mwakilishi Wa Jumuiya Ya Saidia
Wazee Bw.Salvus Duba Ameyataja Matizo Wanayokabiliana Nayo Kuwa Ni Madiwani
Kutohudhuria Katika Vikao Vyao Kutokana Na Kutokuwa Na Posho.
Katika Maadhimisho
Hayo Pia Wazee Wamepewa Vitambulisho Vya Matibabu Bila Malipo
Vilivyotolewa Na Mfuko Wa Taifa Wa Bima Ya Afya Mkoani Hapa.
Kauli Mbiu Katika Maadhimisho Hayo Ni Maisha
Marefu Yanaashiria Ongezeko La Wazee Tuboreshe Huduma Zao.
No comments:
Post a Comment