Wednesday, October 24, 2012

WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA WATU WAZIMA


Story ya Ahmad Nandonde , Munsoma
WANANCHI MKOANI MARA WAMETAKIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA ELIMU YA WATU WAZIMA INAYOTOLEWA NA TASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA TEWW KWANI TAALUMA KUTOKA KATIKA TAASISI HIYO NI  ELIMU KAMA INAYOTOLEWA KATIKA SEHEMU NYINGINE YEYOTE.

AKIZUNGUMZA OFISINI KWAKE HII LEO MKUFUNZI MKAZI WA TAASISI HIYO MKOANI HAPA BW.ERNEST YOHANA AMESEMA KUWA NI WAJIBU WA KILA MMOJA KUPATA ELIMU IPASAVYO KWANI ELIMU INAYOTOLEWA NA TAASISI HIYO HUMUWEZESHA KUPATA NAFASI YA KUENDELEA NA MASOMO  KATIKA ELIMU YA JUU.

AIDHA AMESEMA KUWA PIA KWA MWANAFUNZI ANAPOHITIMU ELIMU YA SEKONDAR HUPATA NAFASI YA ZA KUJIUNGA NA VYUO VYA UALIMU IKIWA NI PAMOJA NA NAFASI MBALIMBALI ZA AJIRA KAMA VILE JESHI,POLISI NA SEHEMU MBALIMBALI ZA AJIRA BAADA YA KUJAZA FOMU MAALUM ZIJULIKANAO KAMA CELL FORM. 

PIA BW.YOHANA AMEWAOMBA WAFANYAKAZI AMBAO HAWAKUBAHATIKA KUPA ELIMU YA SEKONDARI KUJIUNGA NA TAASISI HIYO ILI KUJIENDELEZA ZAIDI KIELIMU KWA LENGO LA KUPANUA WIGO MPANA KATIKA AJIRA ZAO.

MIONGONI MWA MASOMO YANAYOPATIKANA KATIKA TAASISI HIYO NI PAMOJA NA MASOMO YA KOMPYUTA,UDEREVA WA MAGARI PAMOJA NA KOZI ZA HOTLE AMBCHO KINAPATIKANA WILAYANI BUNDA.

No comments: