Saturday, October 13, 2012

WAISLAMU HUISHENI UISLAMU

Story ya Rashid Mtagaluka, Via Facebook


Waislamu kote nchini wamekumbushwa juu ya umuhimu wa kufanya juhudi katika kuuhisha Uislamu sanjari na kujiletea maendeleo katika jamii yao.

Akizungumza leo katika hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi katika shule ya Almustaqiim iliyopo Mtoni kwa Aziz Alli Temeke jijini Dar es Salaam sheikh Mansour Nassor alisema hakuna juhudi kubwa zaidi ya watu kuwarithisha watoto wao elimu.

Kwa upande wake meneja wa shule hiyo ambaye pia ni Amir wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania sheikh Faris Saleh (pichani) aliwataka waislamu kupupia fursa za kuanzisha shule kwa maelezo kuwa shule zilizopo kwa sasa hazitoshi.

mwaka jana shule hiyo ilifaulisha wanafunzi wake wote 18 wa darasa la saba kwa kiwango cha alama A na B. mwaka huu pia wanatarajia matokeo yataendelea kuwa mazuri

No comments: