Saturday, October 13, 2012

KUHUSU VURUGU ZA MBAGALA JANA JIJINI DAR- MDAU AFUNGUKA


 • KUHUSU SUALA LA MBAGALA MIMI MNINUKUU HIVI:
  Mimi ni Muislamu naamini katika sharia na misingi ya kiislamu na Hakuna Tatizo mimi kuwa mwislamu. Na hakuna tatizo katika Uislamu kwa sababu unanifundisha kuheshimu sheria na kumheshimu kila mtu. unaifundisha upendo na huruma.
  Pia Uislamu unanifundisha Kumuamini ALLAH ambae waingereza wanamuita God, waswahili wanamwita Mungu, Wamasai wanamwita NGAI, wa Israel Wanamwita Jehova. Pia hapa Bado sioni tatizo Mungu ndie Allah na Ningekuwa Muisraeli Ningemuita JEHOVA.
  Kubwa zaidi ni kwamba uislamu unanifundisha kuwa na HEKIMA Na SUBIRA. Ila kinachoniuma ni kwamba Watanzania wenzangu tumekosa SUBIRA na HEKIMA pia.
  Kilichotokea huko Mbagala kimelifedhehesha taifa, ni Fedheha kwa Uislamu na pia ni fedhea Kwa Wapenda amani Duniani Kote. Kitendo cha kijana kukidhihaki kitabu Kitakatifu ni jambo linalokera kwa waumin na si Waislamu tu kitendo kile kingefanywa na Mtu mwingine dhidi ya dini nyingine pia kingewakera waumini wa dini husika. Hili ni jambo lisilofichika kwamba Tukio hilo ni Dhihaka Kubwa.
  Lakini Dhihaka hii imetuondolea subira na hekima tuliyonayo waislamu. Kwa kuwa kijana yule tayari alikuwa amekwisha fikishwa chini ya mikono ya dola ilitupasa Tumpe malalamiko yetu Mwenyez Mungu na kusubiri kuona HUKUMU ya ALLAH na Badala yake Tulivunja subira Na Kutaka Kutoa Hukumu tena Bila kufuata sheria. Katiaka hili tulikosa hekima.
  Kibaya zaidi tulitengeneza hisia ambazo pengine si za kweli kwamba kijana huyo ametumwa na waumin wa dini nyingine. Mimi siamin hivyo. Tusipo kuwa makini katika hili tunaweza kulingiza Taifa Machafuko yasiyo ya Msingi. Kwa tarifa ni kwamba tayari kuna makanisa kadhaa yamevunjwa vioo. Sina uhakika kamili kama waliofanya hivyo ni Waislamu.
  Lakini hata wenzetu watakosa hekima kama wataamua moja kwa moja kuamini kuwa makanisa hayo yalishambuliwa na Waislamu.
  Inawezekana kabisa hata yule mtoto hakutumwa mtu bali ilikuwa ni akili ya kitoto tu, au kweli ametumwa na mtu ila Si mkristo wala askofu bali ni raia mmoja tu wa kigeni mwenye malengo mabaya na nchi yetu ili kuipoteza amani tulionayo nchini.
  ifahamike kwamba nchi yetu ina rasilimali nyingi sana na nchi nyingi zinatamani kunyakua lulu iliyopo Tanzania. Walijaribu kutuletea ukabila tupigane vita ili walete majeshi yao wanayoyaita ya kulinda haki za ki binadamu watuibie LULU yetu wakashindwa kutokana na misingi aliyoiweka Mwalimu.
  Wakatulazimisha vyama vingi wakiamini kabisa hatuta dumu katika amani sasa ni takribani miaka ishirini na tunazidi kukomaa kidemokrasia. Njia hii pia ilishindwa kutimiza azma yao ya kuleta machafuko nchini.
  Wakaamua kuuchokonoa Muungano na kupandikiza kero Mbali mbali wakiamini kabisa hatuta dumu Katika Muungano sasa TUnaandika KATIBA mpya inayoenda kujenga muungano Imara zaidi. njia hii pia imeshindikana kuvunja Amani yetu.
  Kwa sasa wamechunguza na kugundua Njia ya kupitia ni Udini. Yaliyotokea Zanzibar Pamoja na hili La Mbagala Yanaweza Kuwa na uhusiano ki Mantiki. Kwamba inawezekana kabisa Wapo baadhi ya watu ( SIO WATANZANIA) wanatumika Katika kupandikiza chuki za Udini kati yetu. Hofu yangu ni kwamba Viongozi pamoja na Waumini wa dini mbali mbali Bado hawajalijua hili.
  Tusipo amua sasa Kuungana na kuzima huu moto wa udini kabla haujapamba utatugarimu baadae. Tujifunze kutokana na makosa ya wenzetu Nigeria tatizo la udini limekuwa SUGU na Gumu Kulingoa. Sisi tuanze sasa kuung'oa huu mti mchanga wa Udini na Tupandikize mti wa umoja Wa kitaifa wenye kufundisha kuheshimu imani ya mtu pamoja na uhuru wa kuabudu.
  Niwatahadharishe "RAFIKI ZANGU" My Sworn brothers pamoja na watanzania kwa ujumla kuwa makini na kauli zenye kejeli juu ya dini fulani ama dhehebu fulani, tuheshimu imani za wengine lakini cha zaidi tuwe wavumilivu na wenye subira naamin MUNGU yupo atatuonesha njia. Naomba nimpongeze shehk wa mkoa wa Dar es Salam kwa Busara Zake.
  Nimalizie kwa kusema MUNGU ni mmoja! Sisi tunamwita ALLAH kwa kiswahili ni MUNGU, Waingereza wanamwita GOD, Wamasai humwita NGAI na Israel Humuita JEHOVA. Mungu ni Mmoja Dini ni mfumo wa maisha Adui yetu ni SHETANI ( Remember The enemy of your enemy is your FRIEND)..Tunajenga Nyumba MOJa Kwa NINI TUGOMBEE FITO?
  WABILLAH TAWFIQ

  MUNGU NIBARIKI MIMI, MUNGU IBARIK TANZANIA, IBARIK AFRIKA IBARIK NA DUNIA.

  AMEN.

No comments: