Sunday, October 14, 2012

MAKONGORO NYERERE APIGWA CHINI CCM

Story ya Ahmad Nandonde , Musoma

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA MARA MHESHIMIWA CHARLES MAKONGORO NYERERE AMESHINDWA KUTETEA KITI HICHO MARA BAADA YA KUBWAGWA NA CHRISTOPHER MWITA SANYA KATIKA UCHAGUZI HUO.

UCHAGUZI HUO UMEFANYIKA OCTOBA 13, KATIKA UKUMBI WA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA SONGE AMBAPO NAFASI HIYO ILIKUA IKIGOMBEWA NA WATU WATATU AMBAO NI ENOCK MWITA CHAMBILI, CHARLES MAKONGORO NYERERE NA CHRISTOPHER MWITA SANYA AMBAYE NDIE ALIIBUKA KIDEDEA KATIKA KINYANGANYIRO HICHO.

MBALI NA KUANGUKA KATIKA UCHAGUZI HUO MAKONGORO AMETUMIA NAFASI HIYO KUWASHUKURU WOTE WALIOMPIGIA KURA NA AMBAO HAWAKUMPIGIA KURA NA KUWATAKA WAONDOKANE NAMAKUNDI YALIYONDANI YA CHAMA HICHO NA KUONDOA SIASA ZA CHUKI ILI KIJENGA CCM IMARA ITAKAYOWAFANYA WASIMAME IMARA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2014 NA 2015.

AIDHA AKIMKABIDHI KITI MWENYEKITI HUYO MPYA WA MKOA WA MARA MAKONGORO AMESEMA KUWA AEPUKE SIASA YA KUYUMBISHWA NA BAADHI YA WATU NDANI YA CHAMA HICHO KWANI KWA KUFANYA HIVYO ATAANDAA MATUNDA MABAYA KATIKA UCHAGUZI WA 2014 NA 2015.

AMEONGEZA KUWA YEYE BADO NI KIJANA MDOGO AMBAE ANAWEZA KUTUMIA NGUVU ZAKE KUONA NA KUTATUA MATATIZO YALIYO NDANI YA CHAMA HICHO BILA KUTIKISWA WALA KUYUMBISHWA NA YEYOTE.

NAE KWA UPANDE WAKE MWENYEKITI MPYA WA CHAMA HICHO BWANA CHRISTOPHER MWITA SANYA AMEWASHUKURU WANACHAMA WA MKOA HUO NA KUAHIDI KUTOA USHIRIKIANO WA KUTOSHA KATIKA UTENDAJI KAZI NA KUAHIDI KUSHUGHULIKIA KWA NGUVU ZOTE SIASA YA MAKUNDI NA CHUKI INAYOENDELE NDANI YA CHAMA HICHO

No comments: