Friday, October 26, 2012

MGODI WATAKIWA KUTOA TAARIFA YA FEDHA YA KILA MRADI NA MISAADA YAOStory ya Ahmad James Nandonde
UONGOZI wa shule za msingi zinazozunguka mgodi wa dhahabu Africa Barrick Gold Mine ( ABG) ulioko Nyamongo Wilayani Tarime wameuomba mgodi huo kutoa taarifa za fedha katika miradi na misaada yao wanayoitoa mashuleni ili kuweka kumbukumbu za shule juu ya miradi iliyotekelezwa na ABG.

Imeelezwa kuwa mgodi wa Barrick umekuwa ukitoa misaada mashuleni kama vile, madawati ,ukarabati wa majengo ya shule na misaada mingine lakini umekuwa hausemi kiasi cha pesa kilichogharamia mradi au msaada pindi unapokamilika na kukabidhiwa shuleni.

Wamesema kuwa wanaushukuru mgodi wa ABG kwa msaada wa madawati mashuleni lakini kuna haja ya mgodi kutoa tarifa za fedha kwa maandishi moja kwa moja wakati wa makabidhiano ili kujiridhisha badala ya kungoja kusikia kupitia vyombo vya habari.

Elisha Nyamhanga mwenyekiti wa kijiji cha Nyangoto-Nyamongo ambacho ni kati ya vijiji vinavyozunguka mgodi amesema kuwa mgodi umekuwa hauwashirikishi viongozi wa serikali ya kijiji mara kadhaa pindi wanapokabidhi miradi kwa wananchi na kuwa pindi wanapowahusisha huwapatia tarifa ya ghafula wanapofika kukabidhi mradi jambo linalowafanya wananchi kulaumu kwa kutoshirikishwa wakati wa makabidhiano ya miradi ili nao wajiridhishe.

Hata hivyo uongozi wa mgodi kupitia Ofisa habari wake Robart Odundo alisema kuwa taarifa za fedha za miradi inayotekelezwa na mgodi kwa ajili ya jamii utolewa kupitia vyombo vya habari.

No comments: