Thursday, October 25, 2012

LIPUMBA AIBUKIA KWENYE SUALA LA KUKAMATWA KWA SHEKH PONDA, A LAANI VURUGU ZILIZOTOKEA..STORY YA RASHID MTAGALUKA
CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMEWATAKA WATANZANIA KUTOKUBALI KUINGIZWA KWENYE MAPAMBANO YA KIIMANI ILI AMANI, UPENDO NA MSHIKAMANO VIENDELEE KUTAMALAKI.

SANJARI NA HAYO, CHAMA HICHO KIMELAANI VIKALI KITENDO CHA KIJANA EMMANUEL JOSEPHAT KWA MAKUSUDI KUAMUA KUINAJISI QUR’AN TUKUFU.
HAYO YAMESEMWA LEO NA MWENYEKITI WA CHAMA HICHO TAIFA PROFESA IBRAHIM LIPUMBA ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI OFISINI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM.

AMESEMA HATUA YA KIJANA EMMANUEL KUKOJOLEA MKOJO QUR’AN NI KIASHIRIO CHA KUONESHA NAMNA MPOROMOKO WA MAADILI KWA TAIFA ULIVYOSHTAD.

HATA HIVYO AMESEMA KITENDO HICHO HAKIHALALISHI KWA JINSI YOYOTE ILE IWAYO NA UVAMIZI WA MAKANISA ULIOAMBATANA NA UHARIBIFU MKUBWA,WA MALI NA KWAMBA ANAHISI NI VITENDO VILIVYOFANYWA NA WATU WAHUNI WALIOJINASIBISHA NA UISLAMU.

AIDHA PROFESA LIPUMBA AMEVISHUKIA VYOMBO VYA DOLA AMBAVYO ALIDAI VINA MCHANGO MKUBWA KATIKA KULINDA AMANI YETU SANJARI NA KUVURUGIKA KWAKE.

AKISHEREHESHA NUKTA HIYO PROFESA LIPUMBA ALITOA MFANO WA KUKAMATWA KWA SHEIKH PONDA ISSA PONDA NA KUHUSISHWA KWAKE NA VURUGU ZA MBAGALA NI USHAHIDI KWAMBA JESHI LA POLISI HALITENDI KAZI ZAKE KWA KUZINGATIA WELEDI.

AMESEMA UNAWEZA USIKUBALIANE NA SHEIKH PONDA KATIKA MAELEZO NA MSIMAMO WAKE KUHUSU DHULMA DHIDI YA WAISLAMU, LAKINI NI MAKOSA MAKUBWA KUMSINGIZIA MAMBO AMBAYO HAKUYATENDA.

AMESEMA KESI YA VIWANJA NI YA MAHAKAMA YA ARDHI, KWAMBA MWENYE KIWANJA KILICHOVAMIWA ALIPASWA KUKIMBILIA MAHAKAMANI NA KUELEZA JINSI KIWANJA CHAKE KILIVYOVAMIWA BADALA YA POLISI KUINGILIA KATI NA KUMKAMATA SHEIKH PONDA NA KUSABABISHA GHASIA KUBWA ZILIZOTOKEA IJUMAA ILIYOPIA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

No comments: