Thursday, October 25, 2012

HAMADI RASHID AULA CHAMA CHA MABUNGE DUNIANI


Mbunge wa Wawi nchini Tanzania kupitia chama cha Wananchi CUF ameteuliwa na Kamati tendaji ya Chama cha Mabunge Duniani (IPU) kuwa mjumbe wa kamati ndogo ya ukaguzi wa ndani kwa mahesabu ya mwaka 2013 ya Chama hicho katika mkutano unaoendelea nchini Canada.

Uteuzi wa Hamad ambaye pia ni mjumbe wa mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani ulifuatia pendekezo la Umoja wa Mabunge ya Afrika lililowasilishwa na Katibu Mkuu wake Koffi N’zii Oktoba 22, 2012, nchini Bangladesh ambapo kikao cha umoja wa mabunge ya Afrika kilimteua Hamad Rashid kuwa mjumbe atakayewakilisha umoja huo kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Mabunge Duniani.

Pamoja naye yupo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mheshimiwa Anne Semamba Makinda na David Kafulilla Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi).

HABARI KWA HISANI YA RASHID MTAGALUKA via Facebook

No comments: