Tuesday, October 2, 2012

HABARI ZILIZO SHIKA VICHWA VYA HABARI LEO KWA KIFUPI HIZI HAPA...

MBEYA: MBUNGE MARY MWANJELWA ANUSURIKA KATIKA AJALI ILIYOUA 9

Watu 8 wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa akiwemo Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa baada ya lori  la mafuta kufeli breki wakati likitelemka mlima wa Iwambi Mji wa Mbalizi na kuyagonga magari matatu ambapo kati ya hayo magari mawili yaliteketea kwa moto .

Imeelezwa kuwa ndani ya gari la Mbunge huyo kulikuwepo na watu wawili dereva wa gari hilo aliyejeruhiwa miguuni na kichwani huku   mwanamke mmoja anayesadikiwa kuwa  ni Katibu wa Mbunge huyo ambaye inadaiwa ameteketea  kwa moto na kubaki mifupa na majivu.

Ajali hiyo ilitokea Jumanne, Oktoba 2, 2012 majira ya saa nane za mchana katika eneo la  Mteremko wa Iwambia mbapo alisema Lory hilo la mafuta likiwa na namba T81 4BTC na tela lenye namba T815 BT linadaiwa kufeli breki na kuyagonga magari matatu likiwemo gari la Mbunge huyo.


Source: http://www.wavuti.com


SEGERA -TANGA... BASI LATEKETEA

Picture

Basi la abiria la kampuni ya Dar Express limepata ajali ya kuungua na kuteketea kwa moto leo asubuhi katika eneo la Segera kwenye njia panda ya Dar es Salaam-Arusha-Tanga.

Basi hilo lilikuwa likitokea Arusha kuelekea Dar es Salaam likiwa na abiria sitini na tano.

Imeripotiwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa au kupoteza uhai katika ajali hiyo isipokuwa mizigo yote ambayo iliteketea.

Basi hilo lilikuwa na wanafunzi. Askari usalama wa barabarani aliyekuwa zamu katika eneo hilo aliona moshi ukitoka na mara moja akawaamuru abiria wote kushuka. Muda mfupi baadaye gari hilo lilishika moto. Gari la zimamoto kutoka Korogwe lilikuwa likitarajiwa kufika katika eneo hilo kutoa msaada wa kudhibiti moto huo

No comments: