Tuesday, September 11, 2012

MAANDAMANO YA WAANDISHI WA HABARI LEO......

>> DAR , MWANZA , IRINGA YAFANYIKA,
>> MUSOMA WAZUIWA , WATANGAZA KUTOANDIKA HABARI ZA POLISI
>> WAZIRI NCHIMBI ATIMULIWA JANGWANI


KATIKA PICHA DAR...


IRINGA


Mmoja wa waandishi wa habari Iringa akilia kwa uchungu baada ya kukumbuka kuwa mnamo march mwaka huu Mwenyekiti Mwangosi alisimama hapo kwaajili ya kuwatia motisha waandishi juu ya uhuru wa habari na kusema "hata kama atakufa lakini anaamini kuwa bado wapo wanahabari watakaokuwepo kutetea maslahi ya wote(Picha kutoka francisgodwin.blospot.com na wavuti.com)

WAZIRI NCHIMBI, Via wavuti
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, amekumbana na fadhaa ambayo haikutarajia wakati alipotimuliwa katika maandamano ya waandishi wa habari ya kupinga mauaji ya mwandishi mwenzao wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, David Mwangosi, wakati alipozuka bila mwaliko.

Huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti, waandishi waliandamana kuanzia kwenye ofisi za Channel Ten katikati ya jiji la Dar es Salaam na kutembea hadi katika viwanja vya Jangawani lakini walipofika mwisho wa maandamano yao walipigwa na butwaa baada ya kumkuta Waziri Nchimbi akiwa wa kwanza kufika katika eneo hilo tayari kupokea maandamano.

Wakati Nchimbi akijiandaa kuanza kuzungumza mbele ya wanahabari, upinzani mkali ukazuka kwa waandishi dhidi ya kiongozi huyo wa serikali wakitaka aondoke mahala hapo kwani maandamano hayo yalikuwa hayamuhusu.

"Atokee.... aondokee.... hatumtakiiii.... nani kamleta hapa?" yalikuwa ni baadhi ya maneo yaliyokuwa wakitolewa kwa sauti kubwa kupinga uwapo wa waziri Nchimbi mahala hapo.

Huku akizomewa, Waziri Nchimbi alijaribu kuvumilia aibu hiyo kwa takriban dakika tano huku pengine akitumai kwamba watamruhusu kuzungumza kilichompeleka mahala hapo.

Mwandishi wa habari mkongwe, ambaye pia ni mwanasheria, Nyaronyo Kicheere, alisogea mbele ya umati wa waandishi na kusimama jirani na alipokuwapo waziri Nchimbi na kusema: "Tumeambiwa tunakuja hapa kwa ajili ya mkutano wa waandishi wa habari na utapokewa na jukwaa la wahariri, inakuwaje tupokewe na mtu mwingine. Hatumhitaji mtu mwingine hapa, aondoke."

Baada ya kauli hiyo, waziri Nchimbi aliondoka mahala hapo na kuzua shangwe kubwa kwa waandishi ambao pia walimsindikiza kwa kumzomea mpaka alipoingia katika gari lake la wizara. Hakuja na gari lake la waziri.

STORY YA AHMADI NANDONDE , KUTOKA MUSOMA

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA KIMEAZMIA KUTOANDIKA TAARIFA ZOZOTE ZA KIPOLISI KUANZIA SEPTEMBA 11 MWAKA HUU.

KAULI HIYO IMEKUJA KUFUATIA AGIZO LA KAMANDA WA POLISI MKOANI HUMO KUZUIA MAANDAMANO YA AMANI YA WAANDISHI WA HABARI YALIYOLENGA KUKEMEA NA KUZUIA MATUMIZI YA NGUVU KAMA YALIVYOFANYWA MKOANI IRINGA NA KUSABABISHA KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MAREHEMU DAUDI MWANGOSI.

AKITOA TAMKO HILO MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WAN HABARI MKOANI MARA BWANA EMMANUEL BWIMBO AMESEMA WAMEAMUA KUCHUKUA MAAMUZI HAYOKUFUATIA HATUA YA JESHI LA POLISI MKOANI HUMO KUZUIA MAANDAMANO YALIYOPANGWA KUFANYIKA HII LEO

AIDHA AMEONGEZA KUWA KUANZIA SASA HAWATAPOKEA WITO WA AINA YOYOTE ILE KUTOKA KWA JESHI LA POLISI MKOANI HUMO KUWAITA WAANDISHI KWA LENGO LA KUWAPA HABARI NA KUSEMA WAWATUMIE WAANDISHI WAO JESHI LA POLISI KUTOA TAARIFA ZAO.

HATA HIVYO BAADHI YA MIKOA MBALIMBALI NCHINI KAMA MKOA WA DAR ES SALAAM IMEENDELEA NA MAANDAMANO YAO KWA AMANI,YAKIANZIA KATIKA KITUO CHA CHANELI TEN ALICHOKUA AKIFANYIA KAZI MAREHEMU DAUD MWANGOSI.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

No comments: