Friday, August 24, 2012

MTWANGO NET ..MTWARA WAELIMISHA WANANCHI JUU YA KATIBA MPYA


Story na Albert Laizer
Wananchi wa Nanyamba katika mkoa wa Mtwara wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao juu ya mabadiliko ya katiba pindi muda utakapofika wa kutoa maoni…
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa mji mdogo wa Nnanyamba Ndg Alli Mpenye alipokuwa akifungua mdahalo kuhusu katiba uliofanyika katika eneo hilo….
Mdahalo huo ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Mtwangonet ulikuwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kuhusiana na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania iliyopo hivi sasa….
Mwezeshaji wa mdahalo huo Ndg Markos Alban amesema zipo  changamoto mbalimbali zinazohitaji kupatiwa ufumbuzi katika katiba ijayo ikiwemo mikataba,umiliki wa taifa pamoja na uhusiano kati ya dola na wananchi…
Mdahalo huo utaendelea tena kesho katika ukumbi wa Pentekoste uliopo katika manispaa ya Mtwara mikindani na wananchi wameombwa kuhudhuria...

No comments: