Mtafiti mkuu wa mbegu za mazao ya mafuta , Dr Omary Mponda akielezea athari za uhifadhi mbaya wa Karanga naathari zitokanazo na uhifadhi huo |
Dr Mponda akisikiliza swali kutoka kwa mdau wa mkutano huo. |
Waandishi wa habari wakipata neno kutoka kwa mkurugenzi wa Kituo cha Naliendele Dr Elly. |
Dr Mponda na waandishi wa habari. |
STORY KIDOGO HII HAPA....
Mkutano wa kujadili jinsi ya kuzuia sumu zitokanazo na
Karanga…umefanyika mtwara leo.
Wataalamu watafiti wa mazao ya mafuta, wa kituo cha utafiti
wa mbegu cha Naliendele kilichopo mkoani Mtwara, pamoja na wadau wamejadili
namna ya kuweza kupambana na sumu ambayo hutokana na uyoga ambao wanautaja kwa
jina la “aflatoxin”.
Mkutano huo umejadili pia namna ya kuondoa ama kudhibiti
sumu kuvu. Wataalamu wanasema sumu hiyo
inasababisha ugonjwa wa kansa ya ini, pamoja na mtindio wa ubongo..
Hizi ni harakati za mwanzo hapa nchini , kwa mara ya kwanza
zilianzia nchini Malawi. Madhara ya sumu hizo yamepelekea vifo vilivyoripotiwa
sehemu mbalimbali, ikiwemo nchini Kenya.
Wanasema gharama za kutibu ni kubwa hivyo ni vyema wananchi
wakachukua tahadhari hasa kwa kukwepa kula karanga ambazo zimeathiriwa..
Karanga zilizoathiriwa na sumu hiyo ni zile zenye UKUNGU,
ambao jamii kwa muda mwingi wamekuwa wakipuuzia.
No comments:
Post a Comment