Tuesday, June 19, 2012

KOCHA MKWASA ABWAGA MANYANGA , TWIGA STARS

Kocha wa timu ya soka ya Taifa ya wanawake Tanzania, Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa amejiuzulu wadhifa wake.

Mkswasa amesema jana usiku kwamba ameamua kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya na pia timu hiyo
 kutothaminiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mkwasa anachukua hatua hiyo, siku mbili tu tangu timu hiyo itolewe katika kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-1, ikifungwa 2-1 Addis Ababa na baadaye 1-0 Jumamosi mjini Dar es Salaam.

Mapema baada ya kufungwa juzi, Mkwasa alisema kwamba timu hiyo haikuwa na maandalizi mazuri na TFF haikuonekana kuijali kabisa. Lakini Mkwasa atakumbukwa mno kwa kuifikisha juu timu hiyo, akiiwezesha kushiriki fainali za Afrika miaka miwili iliyopita nchini Afrika Kusini, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kihistoria.

Source: http://www.wavuti.com

No comments: