Tuesday, June 19, 2012

RAZA: OICITAIMARISHA UCHUMI WA ZANZIBAR

Mwakilishi wa jimbo la Uzini, Mohammed Raza ameiomba Serikali kufikiria tena uamuzi wake wa Zanzibar kutaka kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Kislamu, OIC baada ya kuzuiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akichangia hotuba ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kikao cha Baraza la Wawakilishi, Raza amesema Zanzibar ilitengua uamuzi wa kujiunga na Jumuiya hiyo baada ya Serikakali ya Muungano kuahidi kujiunga na Jumuiya hiyo lakini hadi sasa haijajiunga.

Amesema Zanzibar kutaka kujiunga na Jumuiya hiyo siyo suala la dini, bali ni kutaka kuimarisha uchumi kufuatia misaada ya miundo mbinu inayotolewa na Jumuiya hiyo.

Raza amesema nchi kama vile Uganda zenye Waislamu wachache zimejiunga na Jumuiya hiyo, hivyo ni jambo la kushangaza kuoina Zanzibar imejitoa katika Jumuiya hiyo.

Amesema kama sababu ni Muungano kutojiunga na OIC, basi hakuna haja ya kulazimishana kwa vile ni Muungano wa kuvumiliana na kujadiliana lakini isiwe sababu ya kuizuia Zanzibar kujiunga na Jumuiya hiyo.

CHANZO ZanzibarIslamicNews.wordpress.com

No comments: