Wednesday, June 13, 2012

CHIZI APELEKA MALALAMIKO KWA WAZIRI MKUU KUMPINGA MWAKYEMBE


Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi ambaye hivi karibuni alitenguliwa katika cheo hicho na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe wiki jana, amefikisha ramsi malalamiko yake kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Kwa mujibu wa gazeti la Habari Leo Chizi amewasilisha malalamiko yake kwa Waziri Mkuu akipinga tuhuma zilizoelekezwa kwake na Waziri, Mwakyembe akidai si za kweli na kwamba zimelenga kumshushia hadhi kwa jamii.
Pamoja na barua hiyo, Chizi amewasilisha lundo la vielelezo vikifafanua tuhuma mbalimbali zilizotolewa na Dkt. Mwakyembe dhidi yake, ili kuthibitisha kutokubaliana na tuhuma hizo kwake. Kaimu Mkurugenzi huyo wa zamani wa ATCL alipotafutwa jana ili kuzungumzia suala hilo alikiri suala hilo kuwasilishwa ofisi ya Waziri Mkuu, ingawa hakuwa tayari kulizungumzia zaidi kwa madai kuwa liko kwenye mamlaka za juu sasa.

Tuhuma ya sare za milioni 80/- 

Maelezo ya Chizi kwa Pinda, yanafafanua kwamba ATCL ilinunua loti 30 za vifaa mbalimbali vya wafanyakazi zikiwamo sare zilizotajwa na Dk Mwakyembe kwa thamani ya dola za Marekani 18, 920 na si dola za Marekani 50,000 kama alivyodai Waziri Mwakyembe, hatua ambayo ilifanya ATCL kuokoa zaidi ya Sh milioni 44 kama ingenunua sare hizo nchini kulingana na bei ya ununuzi iliyowasilishwa ATCL.

Tuhuma ya ukodishaji wa ndege 

Anapinga pia kuhusishwa na ukodishaji wa ndege aina ya Airbus ambayo Waziri Mwakyembe alisema haikuwa na sababu ya kukodishwa, akisema ndege hiyo ilikodishwa mwaka 2007 na kufanya kazi hadi mwaka 2008, wakati yeye aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Agosti 2011. Dk Mwakyembe akizungumzia mkataba huo tata wa Airbus, alisema umeifanya nchi kudaiwa Sh bilioni 69 na kusisitiza kuwa kutokana na hali hiyo, Serikali haikuwa tayari kufumbia macho mambo mengine ya ovyo yanayoendelea katika shirika hilo.

BAURA YA KUSIMAMISHWA KWAKE HII HAPA

No comments: