Wednesday, June 13, 2012

AFRIKA KUSINI YAPATA MKUU WA KWANZA WA POLISI MWANAMKE

MKUU WA ZAMANI WA POLISI

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amemfuta kazi Mkuu wa Polisi Generali Bheki Cele, aliyekuwa ametuhumiwa kwa makosa ya rushwa.

Bwana Zuma aliambia waandishi wa habari kuhusu uamuzi wake na pia kuhusu atakayechukua nafasi yake akiwa ni Mangwashi Phiyega, hatua inayomfanya bi Mangwashi kuwa Mkuu wa Kwanza wa polisi mwanamke.

Generali Cele, ambaye mtangulizi wake alifungwa jela kwa tuhuma za ufisadi, alihukumiwa mwezi Oktoba baada ya taarifa kuhusu kuhusika kwake katika kashifa uuzaji haramu wa nyumba za polisi ingawa alikanusha madai hayo.

Inaaminika alihusika na kampeini ya rais Zuma wakati wa kampeini za uchaguzi wa rais mwaka 2009.
MKUU MPYA WA POLISI 
Mwaka jana afisa anayechunguza kesi za ufisadi, Thuli Mandonsela, alisema kuwa nyumba za polisi zilikodiwa kutoka kwenye kampuni moja ambayo ilipandisha bei ya kukodi na kwamba Cele ndiye alihusika na kashfa ya kupandisha bei ya nyumba hizo.

Bi Madonsela ambaye ni mratibu wa malalamiko ya umma alimshtumu Generali Cele kuwa mmoja wa wale waliohusika na kashifa hiyo.

Alichunguza utaratibu wa kukodisha nyumba ambazo zilikuwa za polisi mjini Pretoria na mji wa Mashariki wa Durban na kupata kweli zilipandishwa bei kinyume na sheria.

Chanzo: BBC 

No comments: