Wednesday, May 30, 2012

WANAHARAKATI WAJITOKEZA KUMTETEA MWANAMKE ALIEFUNGIWA RUMANDE YA MHINDI IRINGA

Sakata la mwanamke mjane Edina Panzi(47) kufungiwa katika moja kati ya ofisi za taasisi ya mikopo ya Brac tawi la Iringa taasisi inayomilikiwa na Raia wa India kwa madai ya kushindwa kulipa deni lake kiasi cha shilingi 5800 limechukua sura tofauti baada ya mwanaharakati wa kituo cha msaada wa kisheria wanawake na watoto Bw Jackson Gaso kujitosa kuifikisha taasisi hiyo mbele ya vyombo vya sheria.


Mwanaharakati kutoka kituo cha msaada wa sheria wanawake na watoto mkoani Iringa Bw Jackson Gaso
Gaso amejitokeza kumsaidia mwanamke huyo kama njia ya kupinga vitendo vya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyofanywa na taasisi hiyo ya Brac ambayo ipo chini ya raia wa India.

Hivyo amesema kuwa kituo chake kinajipanga kumfikisha mahakamani mkurugenzi wa taasisi hiyo kwa ukiukaji wa haki za binadamu kama njia ya kusaidia jamii inayonyanyaswa na taasisi hiyo.

Bi. Edina Panzi (47) siku aliyofungiwa ndani ya m,ahabusu za Brac

No comments: