Wednesday, May 30, 2012

SHULE YA MSINGI LILUNGU MKOANI MTWARA YASHINDWA KUFIKIA LENGO

Na Idrisa Bandali, Mtwara

Shule ya msingi Lilungu mkoani hapa, imeshindwa kufikia lengo la kukusanya sh milioni nane sitini na nne elfu na arobaini na nane kutoka wa wadau mbalimbali wa elimu kama ilivyotarajiwa hapo awali.

Hayo yamebainishwa jana katika kikao cha wazazi na waalimu wa shule hiyo kilichofanyika shuleni hapo mapema leo asubuhi.

Imeelezwa kuwa michango iliyokusanywa mpaka sasa ni milioni mbili ,arobaini na moja elfu, hali ambayo imerudisha nyuma harakati za kuendeleza elimu katika shule hiyo.

Aidha kushindwa huko kufikia malengo ya ukusanyaji wa michango hiyo kumetokana na wadau wa elimu wakiwemo wafanyabiashara na makampuni mbalimbali kushindwa kutoa michano yao kama ilivotarajiwa.

Kwa upande wao wazazi wenye watoto katika shule hiyo ya lilungu wameomba kuwepo kwa mkakati maalumu wa kuwaomba wadau mbalimbali wa elimu kuchangia shule hiyo ili malengo yaweze kufikiwa na watoto wapate elimu bora zaidi

Shule ya lilungu imekuwa ikisifika kuwa na mafanikio makubwa kwa kufaulisha watoto katika manispaa ya mtwara mikindani tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.

No comments: