Wednesday, May 30, 2012

NDAZIBULA: VIONGOZI WA USHIRIKA KUWENI MAKINI MLETE TIJA

Na Idrisa Bandali Mtwara

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mtwara ambae pia ni diwani wa kata ya Naumbu, Bw. Mussa Ndazibula, amewataka viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi kuwa makini katika kuongoza wanachama wao ili vyama viwe na tija katika ushirika.

Diwani Ndazibula ameyasema hayo jana katika ufunguzi wa warsha ya siku mbili iliyoanza katika chuo cha ushirika mkoani hapa, inayohusu sheria na taratibu za vyama vya ushirika kwa wanachama wake, na kusema kuwa kiongozi makini ni yule anaye wajali kwanza wanachama wake anao waongoza kwa kulinda maslahi yao na kuwapa misingi ya maadili ya uzalishaji mali.

Aidha diwani huyo amewashukuru viongozi hao kwa utendaji wao mzuri wa kazi katika vyama vya msingi vya ushirika, ambapo sasa amewataka kuwa wepesi katika kuwasiliana na wataalamu wao pindi matatizo yanapotokea ili kuepusha madhatra yasiyokuwa yalazima.

Jumla ya washiriki wapatao 40 wanatarajia kupata mafunzo mbalimbali katika warsha hiyo ikiwemo mafunzo ya sheria, mipango na bajeti.

No comments: