Tuesday, May 29, 2012

MBWA KUANZA KUCHANJWA ... SOON

Na Idrisa Bandali, Mtwara

Picha : MAKTABA

Wizara ya mifugo na uvuvi imetoa tarehe ya kuanza kwa kuchanja maradhi ya mbwa.

Hayo yameelezwa leo na Dr, Mwanaganzala Doto Maziku wakati akizungumza katika washa elekezi ya kuthibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa maafisa wa mifugo na kilimo wa halmashauri za mkoa huu.

Imeelezwa kuwa kuthibiti kichaa cha mbwa ni pamoja na kutoa chanjo kwa mbwa na chanjo kwa binadamu.

Aidha dr ,Maziku amesema kuwa kwa mkoa wa mtwara chanjo ya mbwa itaanza tarehe 18-6-mwaka huu hadi 27-6-katika viwanja vya mashujaa ambapo katika wilaya mafisa mifugo wata panga sehemu elekezi kwa shughuli hiyo.

Mradi huo umeelezwa kuwa upo nchini kwa wilaya 24 kwa mikoa mitano ya Mtwara,Dar-Es-Salaam,Pemba,Morogoro pamoja na Lindi huku halmashauri za wilaya zikitakiwa kutenga fedha zakugharimia chanjo kila mwaka baada ya mradi huu kwisha.

Ugonjwa wakichaa cha mbwa unaathiri binadamu na mifugo na hakuna njia nyingine ya kuthibiti ugonjwa huo ispokuwa kwa njia ya chanjo.

No comments: