Tuesday, May 29, 2012

CHADEMA CHAJIANDAA KUSHIKA DOLA

Na Idrisa Bandali , Mtwara
Chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA, kimeeleza kuwa kimeanzisha kampeni ya movement for change, kwa lengo la kukiandaa chama hicho kushika dola.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama hicho ndugu Freeman Mbowe, wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa mkoani mtwara

Mkutano huo wa hadhara umehudhuriwa na viongozi wote wa ngazi ya juu ya kitaifa wa chama hicho ambapo mbowe ameeleza kuwa ujio huo umelenga kuwaamsha wakazi wa mji huu kabla ya kuelekea kuanza kwa kikao cha bujeti hivi karibuni.

Akizungumia suala la umasikini mwenyekiti huyo ambae pia ni kiongozi wa kambi ya upinzini bungeni amesema Tanzania nzima inamsiba wa masikini ambao umekuwa ukisababishwa na baadhi ya viongozi wa chama tawala kuchezea rasilimali za taifa kwa maslahi yao ambapo amewataka wananchi kukiona chama hicho kuwa ndio mkombozi wao.

Aidha kwa upande wake katibu mkuu wa chama hicho Dk Slaa amesema umasikini umesababishwa na mapungufu ya katiba ambayo mpaka sasa inawanyima haki wabunge kushughulikia suala la matumizi ya fedha za umma.

Dkt Slaa amewataka wananchi pia kuungana na meli ya chadema ikiwa ndicho chama pekee kilicho na matumaini kwa watanzania.

No comments: