Thursday, May 24, 2012

MAKINDA 5 WANAOTARAJIWA KUNG'AA KATIKA MASHINDANO YA EURO 2012

Imeandaliwa na Mdau Charles Abel
euro2012polandukraine1 Euro Cup Soccer 2012

1. Xherdan Shaqir(Uswizi),





Ni miongoni mwa makinda yaliyokosha wapenzi wengi wa soka katika ligi ya mabingwa barani Ulaya huku akivitoa udenda vilabu vikubwa vya soka barani humo,kwa sasa anachezea klabu ya FC Basel ya Uswizi.





2.Alex Oxlade Chamberlain(England),



Ni mchezaji mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kuwachambua wachezaji wa timu pinzani na kupiga mashuti.Ingawa kuitwa kwake kumewashangaza wengi,kinda hili la Arsenal linaweza kuleta msisimko mkubwa katika mashindano hayo.






3,Mario Gotze(Ujerumani).

Huyu ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa cha kusakata kabumbu,ambapo wachambuzi wengi wa soka wamekuwa wakimfananisha na mchezaji wa zamani wa taifa hilo Oliver Bierhoff.



4,Juan Mata(Hispania)





Bila shaka kipaji cha Mata hakihitaji maelezo mengi kwani wengi wameona shughuli yake akiwa na Chelsea,nadhani atang'ara sana kule Ukraine na Poland.






5,Joe Hart(England)


Bila shaka ndiye atakuwa chaguo la kwanza miongoni mwa makipa wa timu hiyo.Uwezo wake uliiwesha timu ya Manchester City kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza

No comments: