Tuesday, March 6, 2012

WANAHABARI IRINGA KUANDAMANA LEO

Maandamano Iringa : March 6, waandishi wa habari mkoani Iringa wanagoma..kushinikiza baadhi ya mambo, wanayoona yanatendwa kinyume na watawala mkoani humo.

Hili ni moja ya mabango yanayotarajiwa kutumiwa leo na wanahabari mkoa wa Iringa wakati wa maandamano yao ya amani ya kupinga ubaguzi wa wanahabari na vyombo vya habari. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo Jukwaa la wahariri wanaunga mkono.
RC Iringa Dkt Christina Ishengoma katika juhudi zake za kutaka kukwepa jukumu la kuyapokea maandamano hayo ya wanahabari , ameshindwa kuwashawishi wayaache maandamano hayo.

No comments: