Wednesday, March 7, 2012

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA AHOFIWA KULIWA NA MAMBA

RPC, LIBERATUS BARLOW , MWANZA

  Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondary Nyamatongo kata ya Nyamatongo wilayani sengerema mkoani mwanza, anahofiwa kuliwa na mamba katika ziwa, viktoria

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani mwanza Philip Kalangi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na amemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Sungwa Jamhuri mwenye umri wa miaka, 18, Tukio hilo lililotokea siku ya tarehe 3 mwezi huu, linamhusisha kijana huyo aliyeenda kuvua samaki katika ziwa viktoria, ndipo alipokamatwa na mamba huyo.

Taarifa za mamba huyo kumkamata Sungwa zimetolewa na wananchi waliokuwa karibu naye wakati akikamatwa, na kwamba jeshi la polisi mkoani mwanza linaendelea na juhudi za kuutafuta mwili wake.

No comments: