Wednesday, March 7, 2012

POLISI MWANZA INAWASHIKILIA WAWILI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI


RPC MWANZA

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linawashikilia Watu Wawili kwa tuhuma za Kushiriki Katika Ujambazi, Uliofanyika Katika Kijiji Cha Kabila Kata Ya Kinguru Wilayani Magu, Mkoani Mwanza

Kaimu Kamanda Kalangi, amewaambia waandishi wa habari leo ofisini kwake kuwa, tarehe 3 mwezi huu majira ya saa 8 usiku, watuhumiwa hao walivamia katika kijiji hicho na kufanikiwa kupora bunduki aina ya raifo yenye namba 73526/05385, risasi 2, na sh: elfu 70, mali ya modester thomasi

Wanathumiwa pia kuvamia kwa Nyanda Mageleja na kupora sh: milioni 2 na laki 3, kisha kupora kiasi cha Sh: Elfu 80 kwa Bugumba Makanika.

Watuhumiwa watafikishwa mahakani pindi upelelezi wa kipolisi, utakapokamilika

No comments: