Tuesday, March 6, 2012

IRINGA... KIMYA KIMYA KWA AMAAAANI... WANAHABARI WAMEANDAMANA LEOWANAHABARI WALIOANDAMANA LEO MKOANI IRINGA, KUPINGA
KUNYANYASWA NA OFISI YA MKUU WA MKO HUO KUPITIA
 KWA AFISA HABARI WAKE
 Zaidi ya wanahabari 60 wameandamana kwa amani mkoani Iringa kupinga ubaguzi unaofanywa na idara za serikali kwa  kubagua vyombo na wanahabari katika "coverage" ya matukio mbali mbali.

Maandamano hayo yamefanyika mapema leo, huku wanahabari hao wakiwa wamefunga plasta kuashiria kutotaka kuongea lolote, yalisababisha shughuli za wananchi wengine kusitishwa huku baadhi yao wakiyaunga mkoni.

Ingawa maandamano hayo yalitarajiwa kupokelewa na mkuu wa Mkoa Chrstina Ishengoma, alikataa wajibu huo na ikabidi mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Iringa IPC, Bw Daud Mwangosi.. akawa mgeni Rasmi.... wito wake ukawa ni huuhapa

"...wengi wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya maandamano hayo huku baadhi ya watu wakidhani wanahabari hao wanaandamana kwa ajili ya kutetea kulipwa posho na baadhi wahusisha maandamano hayo na itikidi za kisiasa na kuwa maandamano hayo hayakuwa na mitazamo hiyo kama wanavyofikiri bali ni maandamano ya kupinga manyanyaso dhidi ya wanahabari na ubaguzi dhidi yao..."

Pia alitaka wanahabari mkoani Iringa kutokubali kuendelea kunyamaza kimya kwa ubaguzi unaofanywa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa pamoja na ofisa habari wa ofisi hiyo Denis Gondwe

No comments: