Tuesday, March 6, 2012

CONGO BADO SI SHWARI.....

Majeruhi wa milipuko ya mabomu nchini Congo wakiwa katika
moja ya vituo vya uokozi.

Taarifa kutoka Congo zinaeleza kuwa bado ni hatari kuingia eneo ambapo milipuko ilitokea siku ya Jumapili katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville. Waokoaji huku wakiendelea na juhudi za uokozi wanasema kufikia sasa bado kunamilipuko midogo midogo ambayo ingali inashuhudiwa.
inahofiwa kuwa kuna mamia ya maiti ambazo huenda zingali katika vifusi vya majengo yalioporomoka kutokana na milipuko hiyo ya Jumapili.

Serikali inasema idadi ya waliofariki ni 146 . Hata hivyo takwimu kutoka vyumba vya kuhifadhia maiti na madaktari wanasema kuwa idadi ya waliofariki imefikia zaidi ya 200 na wale waliojeruhiwa ni 1,500No comments: