Tuesday, March 6, 2012

POLISI WANNE (4) TABORA WAFUKUZWA KAZI

RPC ANTHONY RUTHA -- MKOA TABORA
Jeshi la Polisi mkoani Tabora limewafukuza kazi askari polisi wanne wilayani Urambo na kuwafikisha mahakani kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo raia mwema wa mjini Urambo mkoani humo.

Askari hao wakituo cha polisi Urambo wanatuhumiwa kumshambulia kwa kipigo Hassan Mgalula mnamo februari 18, mwaka huu mjini Urambo, na mnamo februari 22, mwaka huu akiwa katika hospitali ya wilaya akipatiwa matibabu, mtu huyo alifariki dunia.

Kwa mujibu wa Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Yassin Mruma waliofukuzwa kazi ni G. 3037 PC Aidano, G. 3836 PC Jonathan, G. 4836 PC Mohamed na G. 5382 PC Akimu, wote walikuwa wakilitumikia jeshi la polisi katika kituo cha polisi Urambo mjini.


Hatua hiyo ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kuwafukuza kazi askari wake wanne inakuja kufuatia shinikizo la wananchi wa mji wa Urambo kuandamana hadi kituo cha Polisi wakitaka askari waliohusika na mauaji hayo wachukuliwe hatua.

No comments: